Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, April 29, 2012

Tigo Yadhamini Siku ya Taaluma kwa Vyuo Vikuu

Tigo Yadhamini Siku ya Taaluma kwa Vyuo Vikuu
Wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali na vyuo watapata fursa ya  kujumuika pamoja katika siku ya Taaluma iliyodhaminiwa na Tigo, na kupata fursa ya kukutana na waajiri wa makampuni mbalimbali kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa nane mchana katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa.
Vyuo vitakavyohudhuria ni pamoja na Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Ardhi, Chuo cha Ardhi, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na vinginevyo. Wanafunzi watakuwa na nafasi ya kufahamiana, kupata taarifa za taalum na kupata taarifa moja kwa moja kutoka kwa waajiri ambao watakaokuwepo katika siku ya maendeleo ya taaluma.
 “Katika uchumi wa leo kuna changamoto nyingi, makampuni lazima yavute watu wenye vipaji bora ili kuendeleza ushindani. “Tukio hili linawasaidia waajiri kuangalia watu wenye vipaji zaidi,” alisema Alice Maro ambaye ni Afisa Uhusiano wa Tigo. ‘’Vijana wenye taaluma na motisha mbalimbali na wanafunzi wapya wanaweza wakajaribu taaluma wanazozipata darasani katika mazingira halisi ya kazi (Kwa vitendo) kwani wanaweza kuwa sehemu za hizo kampuni siku za karibuni’’ alisema.
Burudani ya moja kwa moja kutoka bendi za muziki wa hapa nyumbani itatolewa na Mapacha Watatu na wasanii mbalimbali kutoka Chuo cha IFM wakati wote wa tukio na baada ya hapo wanafunzi watajumuika pamoja katika ukumbi wa Cine Club.




0 comments:

Post a Comment