Help Children
Love them
Saidia Watoto

Friday, April 13, 2012

Mbunge Barwany atoa wito wa watu kujitokeza kushiriki matembezi ya hisani

Ndugu Mtanzania,                                         

YAH: NIFAHAMU

Rejea kichwa cha habari hapo juu. Naandika kukuomba mtanzania mwenzangu kuungana na mimi kwa kushiriki kwenye kampeni ya Nifahamu. Lengo kuu la kampeni hii ni kuelimisha jamii kuondokana na mtazamo hasi kwa walemavu wa ngozi nchini ambao umekuwa ukiendelea kwa miaka mingi sasa.

Mtazamo huu umechangia kuleta maafa mbalimbali kwa walemavu wa ngozi, kwa mfano: mauaji ya kikatili, kukatwa kwa viungo vyao na hivyo kuwaongezea ulemavu zaidi, kutengwa na kutohusishwa kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii,kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni.

Walemavu wa ngozi wanachangamoto nyingi sana katika jamii. Ukiachana na mtazamo hasi, wanakumbwa na majanga mengi yafuatayo: hatari ya ugonjwa wa saratani ya ngozi, imani potofu, uoni hafifu na jamii kuwa na  uelewa mdogo juu ya ulemavu wa ngozi.

Nikiwa miongoni mwa walemavu wa ngozi, nimeanzisha  shirika lisilo la kiserekali (BADEF) linalohusika na kuleta ustawi kwenye maisha ya walemavu wa ngozi nchini.

Tumezindua kampeni hii tukiwa na ujumbe ufuatao:

a)Nilinde – Nina haki ya kuishi kama binadamu mwingine yeyote, pia nahitaji hifadhi ya maisha yangu.       

 b)Nijali – Ninastahili heshima, kuthaminiwa na kupewa huduma na mahitaji           maalumu
c)Nielimishe – Niwezeshe kujitambua, na kujilinda na jamii initambue na kunilinda
d)Naweza – Ninastahili kupewa fursa kama binadamu mwingine yeyote
e)Nipende – Mimi ni mwanadamu kama mwingine yeyote na ninastahili furaha, mapenzi na huruma.


Jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi inatengwa na kunyanyasika sana. BADEF, kwa kutambua hilo imeandaa matembezi ya hisani yenye lengo la kukusanya kiasi cha fedha cha Tsh. Milioni 500 kwa ajili ya kuchangia ili kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini kupitia njia zifuatazo:
a).Kufanya tafiti mbalimbali juu ya hali ya watu wenye ulemavu wa ngozi kv. Kielimu, kiafya na kijamii;
b).Kutoa elimu ya ulemavu wa ngozi;
c).Kuhamasisha ujumuishwaji kwenye sekta mbalimbali nchini na;
d).Kutoa vifaa vya kukinga


0 comments:

Post a Comment