Help Children
Love them
Saidia Watoto

Monday, April 16, 2012

Albino wapewe msaada maalum shuleni-- Mbunge Barwany

Walimu wa shule za msingi na za awali wanahitaji msaada kutoa msaada maalum kwa watu wenye ulemavu wa ngozi, Albino, hususan wakati wakiwafundisha madarasani.

 Wito huo ulitolewa juzi na Mbunge wa Lindi Mjini Salum Barwany wakati akiendesha haramabee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuisaidia Taasisi yake ya Badef inayoshughulikia watu wenye ulemavu wa ngozi.

Alisema kuwa Albino wanakabiliwa na changamoto ya kutokuona mbali hivyo wakiwa darasani hushindwa kuona kile ambacho kinafundishwa ubaoni na hivyo kuwaweka katika wakati mgumu wa kushindwa kufuatilia masomo vema.

Alisema kuwa hali hiyo ni changamoto kwa Albino kwa kuwa wanashindwa kuelewa na pengine kujikuta wakishindwa kufanya vema darasani.

Alifafanua kuwa wananchi wanahitaji kuelimishwa namna ya kuwasaidia na kuwachangia Albino hao ili waweze kusoma kwa kuwapatia michangapo mbalimbali kama vile miwani na vinginevyo.

Pia alisema kuwa wanajamii wanatakiwa pia kuelimishwa zaidi ili waweze kujua namna ya kuwasaidia Albino katika masuala mbalimbali ambapo alitolea mfano kuhusu namna ya kuwalea na kuwatunza Albino wakiwa tangia watoto.

Alisema kuwa elimu katika ngazi ya familia ni kitu muhimu kwa Albino hao na kuwataka wanajamii kuwasaidia kwa hali na mali.

" Najua ni kwamba sisi Albino tumetokana na ninyi watu msiokuwa Albino, hivyo kututenga na kutunyanyasa sio sawa kwa kuwa sio sisi tuliotaka kuwa hivi ila ninyi ndio mliotuzaa naomba muelewe hiolo kwanza" alisema Barwany.

Mtandao huu unatambua juhudi za mbunge huo katika kusaidia jamii ya Albino wenzake hususan katika nyanja ya elimu

0 comments:

Post a Comment