Help Children
Love them
Saidia Watoto

Tuesday, February 21, 2012

THT ambao ni watendaji wakuu wa mradi wa Zinduka waanza kutoa elimu ya Maralia kanda ya Ziwa


Ziara hiyo imedhaminiwa na Africa Barrick Gold


 Wakitumia sanaa za maonesho kutoa ujumbe wa Malaria
Waelimishaji wakiwauliza maswali watoto hao


Na Evance Ng’ingo
KUNDI la Tanzania House of Talent (THT) limeanza ziara ya siku 60 kwa mikoa ya kanda ya Ziwa ambapo wanatumia sanaa ya maonesho kuelimisha kuhusu ugonjwa wa Malaria.

Ziara hiyo inahusisha mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera na  Shinyanga ambapo wasanii hao wanafika mpaka wilaya za vijijini kuelimisha wanafunzi na wanajamii juu ya ugonjwa huo.

Akizungumzia ziara hiyo meneja wa mradi wa Zinduka unaoratibu zoezi hilo, Sadaka Gandi alisema wasanii wanane wapo katika msafara huo.

Alisema kuwa wasanii hao watatumia snaaa ya maigizo, nyimbo pamoja na muziki wa asili katika kufikisha ujumbe.

Alisema kuwa kwa kutumia sanaa THT imeweza kuifikia idadi kubwa ya wanajamii na kufanikiwa kuwaelimisha juu ya maambukizi ya ugonjwa wa malaria na namna ya kujikinga nao.

Alisema kuwa ziara hiyo inatarajiwa kumalizika machi 22 mwaka huu baada ya kuzungukia mikoa yote na kutoa elimu husika ya malaria.

“ Kupitia mradi huu wa utoaji wa elimu ya Malaria kwa njia ya sanaa wasanii wameweza kulifanikisha zoezi hili kwa hali ya juu kwa kuongeza hamasa ya wananchi katika kushiriki vita dhidi ya ugonjwa huu” alisema Sadaka.

Zaiara ya wasanii hao imeanzia na mkoani  Mara ambapo wametembelea shule mbalimbali za sekondari na kuanzisha klabu za wanafunzi zenye majukumu ya  kupambana na ugonjwa wa Malaria.


Wasanii wa THT waliopo katika ziara hiyo ni wale wanaojishughulisha na uchezaji wa aina mbalimbali za ngoma na kuimba.
Mwisho



0 comments:

Post a Comment