Help Children
Love them
Saidia Watoto

Monday, February 20, 2012

Kamati ya vazi la taifa yatoa somo kwa wadau wa vazi hilo


KAMATI inayoshughulikia vazi la taifa imeeleza kuridhishwa kwake na maendeleo ya mchakato wa kutafuta vazi hilo.

Akizungumza katika mkutano na wadau wa sanaa ya ubunifu Mwenyekiti wa kamati ya vazi la taifa Ndesamburo Merinyo alisema kuwa wadau wengi wamejitokeza kufanikisha upatikanaji wa vazi hilo.

Merinyo alisema kuwa wadau hao ni pamoja na wachoraji wa michoro ya mavazi  na pamoja wa wadau wengine.

Alisema kuwa kwa sasa wamepata michoro mingi kutoka kwa wachoraji mbalimbali ambao wamekuwa wakielezea namna amabcho kitambaa cha vazi la taifa kinatakiwa kuwa.

Alisema kuwa kabla ya kupatikana kwa vazi la taifa kwanza kunakuwa na kitambaa cha vazi hilo ambacho ndio kitatumika kupata vazi lenyewe.

 Alisema kuwa tayari kamati yake imeendesha midahalo mbalimbali ikiwashirikisha wadau wa ubunifu, mavazi na sanaa kiujumla na tayari imekusanya mawazo yao kuhusiana na vazi hilo.

“ Ni kwamba kwa sisi kama kamati tunaona kuwa zoezi hili litakuwa ni lenye mafanikio makubwa kwa kuwa mwamko kutoka kwa watanzania ni mkubwa na safari hii kazi takamilika kama ilivyopangwa” alisema Merinyo.

Kamati ya vazi la taifa iliundwa mapema mwaka huu na waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Emanuel Nchimbi kwa lengo la kutafuta vazi la taifa litakalotambulisha taifa la Tanzania.

Katika mdahalo huo wa basata wadau mbalimbali walitoa mawazo yao kuhusiana na wanavyotaka kitambaa hicho kuwa
Mwisho

0 comments:

Post a Comment