Help Children
Love them
Saidia Watoto

Wednesday, July 3, 2013

Vyuo vya Amali Zanzibar kuimarishwa

SUZA
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali imesema itaimarisha vyuo vya amali, ili kukidhi malengo yake ya kutoa ajira kwa vijana wa Unguja na Pemba kuwa wajasiriamali.

  Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Zahra Ali Hamad wakati akijibu Swali la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi, Saleh Nassor Juma (CUF) aliyetaka kujua mikakati ya kuimarisha vyuo vya amali pamoja na kuvilinda na tatizo la uvamizi kwa kujenga uzio.

Akifafanua alisema vyuo vya amali vilivyopo Mkokotoni kwa upande wa Unguja na vitongoji kwa Pemba, vimefanya kazi kubwa ya kusaidia vijana kupata elimu, ambayo itawawezesha kujiajiri na kuacha kutegemea ajira Serikalini.  

Alisema katika Chuo cha Amali kilichopo Vitongoji,  kimekuwa kikitoa mafunzo na taaluma ya mambo ya umeme na Mkokotoni ambacho kinatoa mafunzo ya mambo mbalimbali, ikiwemo ufundi seremala na mambo ya mapishi.  

Aidha, alisema katika mikakati ya kuwawezesha wanafunzi hao kujitegemea, wanatarajiwa kupatiwa mikopo ambayo itawawezesha kujitegemea katika miradi yao wakati wanapomaliza masomo yao.  

 Alisema katika mikakati ya kuimarisha Vyuo hivyo,Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali inakusudia kujenga uzio vyuo hivyo ili kuepuka tatizo la uvamizi linalofanywa na wananchi kutokana na kasi ya ujenzi holela. 

  Hamad alikiri tatizo la uvamizi wa majengo ya Wizara ya Elimu, ikiwemo Shule za Msingi na Sekondari katika Unguja na Pemba kwa kuzipatia hati za umiliki.   

Mradi wa Vyuo vya Amali nchini,  lengo lake kubwa kuwawezesha vijana kujiajiri unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADfB), ambapo tayari vipo jumla ya vyuo vya amali vitatu Unguja na Pemba. 

0 comments:

Post a Comment