Help Children
Love them
Saidia Watoto

Saturday, July 13, 2013

Duh! aisee yani vyeti 677 feki vimekamatwa

OFISI ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa Umma imekamata jumla ya Vyeti vya Kughushi 677 ambavyo wahusika wanadai kuvipata kutoka Wakala wa Usajili, Vizazi na Vifo (RITA), Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).

Vyeti hivyo vimepelekwa katika taasisi hizo ili kujiridhisha kabla ya kuwashtaki kutokana na kuwa Ofisi hiyo haina mamlaka ya kuwashtaki wenye vyeti ambao hawakupata nafasi hizo.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Msemaji na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa ofisi hiyo, Riziki Abraham.  Alisema tangu kuanza kazi kwa sekretarieti hiyo ya ajira, wameendesha mchakato wa ajira kwa waombaji 4,891 na kuwapangia vituo vya kazi.

Alisema kwa mujibu wa sheria, mtu yeyote atakayethibitika  kughushi nyaraka hizo ataweza kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini ya Sh.milioni moja au adhabu zote mbili kwa pamoja.

Pia alisema Sekretarieti ya ajira inaandaa utaratibu wa kutowaruhusu kufanya usaili mwingine waombaji ambao hawatakwenda kuripoti sehemu za kazi walizopangiwa bila kutoa sababu za msingi.

Alisema kutoripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa ni kosa na kuwataka waombaji wa fursa za ajira kutochagua maeneo ya kufanyia kazi, hususan waliopangiwa vituo na Sekretarieti hiyo.

Abrahamu alisema Sekretari ya Ajira kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ilipeleka muswada Bungeni unaopendekeza kukasimu madaraka ya kuendesha mchakato wa ajira ili baadhi ya waajiri wakasimiwe madaraka hayo ili kurahisisha utendaji kazi katika kushughulikia machakato wa ajira kwa baadhi ya kada.

“Huku Sekretarieti ya Ajira ikiendelea kuhakikisha kuwa jukumu hilo linaendelea kutekelezwa kwa ufanisi kwa kutumia kitengo cha udhibiti na ubora kinachosimamia suala zima la uhakiki wa taarifa za mhusika ikiwa ni pamoja na uhakiki wa vyeti,” alisema Abraham.

Aliongeza kuwa, nafasi za kazi zitakazotangazwa na mchakato wake kuweza kukasimiwa ni pamoja na kada ya wasaidizi wa ofisi, wahudumu wa afya, madereva, maofisa watendaji wa Kata, Mtaa, Kijiji, wapishi, walinzi na madobi.

Alisema wengine ni wasaidizi wa kutunza kumbukumbu pamoja na Makatibu Muhtasi walio chini ya cheo cha mwandishi mwendesha ofisi au kada zingine ambazo katibu wa Sekretarieti ataona inafaa kukasimu.

Aidha, alitumia fursa hiyo kuwashauri wanafunzi walioko shuleni na wanaotarajia kuingia vyuoni kuchukua masomo ama kozi za fani ya afya, elimu, mifugo na kilimo akisema maeneo hayo bado yana fursa nyingi za ajira serikalini na wahitimu wake hupangiwa vituo vya kazi kazi moja kwa moja bila kupitia mchakato wa ajira kwenye Sekretarieri.

Aligusia pia mtindo ulioibuka wa watumishi katika sekta binafsi kufanya wizi na baadaye kwenda kuomba kazi katika utumishi wa umma, akisema wameandaa utaratibu wa kuweka matangazo yaliyotolewa ya wizi kama kumbukumbu yao ili wahakikishe wanaajiri watumishi wa serikali wenye weledi na maadili mema.

“Tunachofanya ni kukusanya kumbukumbu kwa waliotuhumiwa na kuwafuatilia wakileta maombi ya kazi kama walituhumiwa isivyo au walishtakiwa na kama tatizo liliisha kwa lengo la kutoingiza katika ajira ya utumishi wa umma watu wenye tuhuma mbalimbali,” alisisitiza

Kuhusu wananchi kupata taarifa kwa haraka juu ya ajira katika utumishi wa umma, alisema ili kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia ya habari na mawasiliano nchini na duniani, Sekretarieti ilianzisha tovuti yake ambayo tangu kuzinduliwa Aprili 2013 imetembelewa na wadau zaidi ya milioni 3.1.

Abrahamu alisema pia wameanzisha Kanzidata za aina tatu ambazo ni za wahitimu wa vyuo, kanzidata ya waliofaulu usaili pamoja na ya waliopangiwa vituo ili kuwezesha nafasi ikitokea ya waliofaulu, lakini hawajapangiwa vituo kupangiwa vituo bila kuanza mchakato upya.

“Jambo lingine ni kuwa sekretarieti ya ajira iko katika hatua za awali za mchakato wa kuwawezesha waombaji wa fursa za ajira kuwasilisha maombi ya kazi kwa mfumo wa kielektroniki kwa nafasi zitakazotangazwa,” alisema

Abraham alisisitiza kuwa hiyo itasaidia kurahisiha kupunguza mlolongo wa kuendeshaji mchakato wa ajira ulivyo sasa, ku

0 comments:

Post a Comment