Help Children
Love them
Saidia Watoto

Wednesday, May 22, 2013

Msanii Niki wa Pili ajiunga na harakati za elimu


MSANII wa muziki wa kizazi kipya Nicki wa Pili ameelezea nia yake ya kuandaa mradi maalum wa kusaidia vijana katika masuala ya elimu.

Ni wa Pili alisema kuwa anatarajia kuanzisha kitu kama vile kijiji cha elimu ambapo vijana watakuwa wakikutana kujadili masuala ya elimu.

Alisema kuwa pitia mradi huo vijana wataongeza hamasa ya kujisomea kwa kuwa watakuwa wakikutana muda wote kujadili masuala ya elimu.

" Mradi huu utafanyikia hapa Dar es salaam na ndio itakuwa ni njia rahisi ya kuwaongezea hamasa sio tu wanafunzi bali hata wazazi wao ambao wengine hawajahamasika katika masuala ya elimu"alisema Niki wa Pili.

Aliongeza kuwa kufeli kwa wanafunzi kunatokana na kukosekana sio tu kwa msukumo kwenye jamii lakini pia hata kukosekana kwa mkakati endelevu wa kuwasaidia vijana hao.
===========

0 comments:

Post a Comment