Help Children
Love them
Saidia Watoto

Thursday, May 2, 2013

Chuo cha kipekee cha Mipango kutimiza miaka 35


CHUO  cha Mipango ya Maendeleo Vijijini ,kilichopo mkoani Dodoma mwakani kinaadhimisha miaka 35 tangu kuanzishwa huku kikiwa chuo pekee  chini ya Baraza laTaifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kutoa shahada  ya uzamili  bila kushirikiana na vyuo vingine.

Hatua hiyo imefuatia baada ya  kuanzia Agosti ,mwaka jana kupandishwa hadhi toka chuo kinachotoa kiwango cha juu cha Shahada (NTA 8) na kuwa na uwezo wa kuendesha Programu mbalimbali za Uzamili ( NTA 9).


Kaimu Mkuu wa Chuo hicho  Profesa  Innocent  Zilihona alisema kwa sasa wana uwezo wa kutoa shahada za uzamili  za aina mbili huku kikiwa chuo cha kwanza kilicho chini ya NACTE kupandishwa hadhi bila kushirikiana na vyuo vingine.


Anabainisha kuwa kuna Vyuo kama IFM na DIT wanatoa shahada hizo lakini hawaendeshi wenyewe bali kwa kushirikiana na vyuo mbalimbali vikiwemo vya nje.


“chuo hiki kila kitu tunafanya wenyewe bila kushirikiana na chuo chochote cha nje kuendesha program hizi jambo ambalo hata NACTE wanajivunia maendeleo ya chuo hiki”Alisisitiza
Alisema chuo  hicho kilianza kutoa mafunzo ya muda mrefu ya miaka mitatu ya  Stashahada ya Juu katika Mipango ya Mikoani  mpaka sasa wanatarajia kuongeza kufikia Programu 17.



Pia kutokana na mahitaji ya shahada ya uzamili wanatarajia kuanzisha program za jioni kwa watu walioko makazini kupata muda kusoma baada ya kumaliza kazi kama ilivyo katika baadhi ya vyuo.


Naye,Makamu Mkuu wa Chuo -Mipango,Fedha na Utawala Tiberio  Mdendemi  alisema  mwaka huu chuo hicho kinaanza maadhimisho ya  miaka 35 kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kufanya kongamano kubwa la Wataalamu  Mipango  ifikapo Februari 1,2014.


Mdendemi  anasema katika maadhimisho hayo shughuli mbalimbali zitafanyika katika kuhakikisha taaluma ya mipango inapewa  nafasi  yake na kujitegemea na siyo kuunganishwa katika taaluma nyingine.
Katika miaka hiyo   chuo  kimeanzisha kituo cha Kanda ya Ziwa - Mwanza kwa ajili ya kuendesha   mafunzo, kufanya utafiti na kutoa ushauri na uelekezi katika masuala ya Mipango ya Maendeleo.


Mdendemi alisema  katika kituo hicho wanatoa Cheti na Diploma  huku wakiwa na wanafunzi 670 wakitumia majengo ya kupanga ya Kanisa la African Inland Church (AIC) huku wakiwa na mikakati ya kujenga majengo yao siku zijazo.


Anasema chuo kina maeneo mengine wanayotarajia kutanua chuo katika eneo la Miyuji Kaskazini  ambazo ni Ekari 40 watakapojenga majengo mengine ya taaluma huku wakitafuta eneo la Chigogwa yenye ekari 200 na tayari mipango ya kupima inaendelea.


0 comments:

Post a Comment