Help Children
Love them
Saidia Watoto

Monday, August 20, 2012

Zantel yasherehekea sikukuu ya Iddi na watoto wa kituo cha watoto yatima, pia yawapatia vifaa vya kujifunzia

Watoto wa kituo cha Al-Husein cha Magomeni wakicheza pamoja na mchekeshaji huyu wakati wa sherehe ya idi pili iliyoandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zantel ikiwa ni ishara ya upendo kwa watoto hao. Tukio hilo lilifanyika katika ofisi za Zantel zilizopo drive inn.

Ofisa uhusiano wa Zantel Jackline Mattowo akiwakabidhi watoto wa kituo cha Al-Husein bandama wakati wa sherehe ya idi pili iliyofanyika katika makao makuu ya Zantel.Kampuni ya Zantel iliwaandalia watoto hao sherehe ya iddi pili kama ishara ya upendo.
Wachekeshaji mahiri wa kundi la Mizengwe, Hemed Maliyaga maarufu kama Mkwere na Jesca Kindole maarufu kama Safina wakiwachekesha watoto waliohudhuria hafla ya sikukuu ya iddi iliyofanyika jana katika ofisi ya Zantel.

0 comments:

Post a Comment