Help Children
Love them
Saidia Watoto

Wednesday, August 22, 2012

UMOJA WA WANAFUNZI WATANZANIA WANAOSOMA KENYA WACHANGIA KAMPENI YA UJENZI WA HOSTELI ZA WASICHANA


Meneja habari wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Sylvia Lupembe Gunze akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kampeni ya ujenzi wa hosteli za wasichana.Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi. Rosemary Lulabuka akifuatiwa na Mwenyekiti wa Wanafunzi wanaosoma nchini Kenya katika chuo cha United States International University (USiU) waliofika kutoa mchango wao katika ofisi za Mamlaka ya Elimu Tanzania.

Mwenyekiti wa Wanafunzi wanaosoma nchini Kenya (USiU) Esther Lugoe akimkabidhi Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Elimu Bi. Rosemary Lulabuka Kiasi cha awali cha shilingi 300,000 ambapo wanafunzi hao wanakusudia kuchangia jumla ya shilingi 500,000 katika kampeni hii.
Mwenyekiti wa wanafunzi wanaosoma katika chuo cha USiU nchini Kenya akielezea wao kama wanafunzi walivyoguswa na mradi huu na kutoa hamasa kwa wadau mbalimbali wa elimu nchini na nje ya nchi kujitoa kwa chochote walichonacho katika kufanikisha ujenzi wa hosteli za wasichana kampeni inayoendeshwa na mamalaka ya elimu Tanzania.
Mwenyekiti wa Wanafunzi wanaosoma nchini Kenya (USiU) Esther Lugoe akimkabidhi Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Elimu Bi. Rosemary Lulabuka Kiasi cha awali cha shilingi 300,000 ambapo wanafunzi hao wanakusudia kuchangia jumla ya shilingi 500,000 katika kampeni hii. habari kalimi Kampeni ya Mamlaka ya Elimu Tanzania inayoendelea ya kuchangisha fedha na vifaa kwa ajili ya ujenzi wa hosteli za wasichana imeendelea kupata mwitikio chanya kutoka kwa wadau mbalimbali wa elimu ambapo leo wanafunzi watanzania wanaosoma nchini Kenya katika chuo cha United States International University (USiU) kupitia mabalozi wa TEA wamechangia shilingi 300,000 katika kuunga mkono juhudi za mabalozi hawa wenye kauli mbiu “Elimu Yao, Wajibu Wetu” kuhakikisha TEA inakamilisha mradi huu. Akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania,Rosemary Lulabuka mchango, Mwenyekiti wa umoja huo Esther Lugoe wamesema wao wameguswa kwa namna ya pekee na matatizo yanayowakumba wanafunzi hasa wa kike kwa kukosa mazingira salama yanayoweza kuwafanya wasome vizuri na lengo lao ni kuchangia shilingi 500,000 kwa hiyo hiyo laki mbili italetwa ndani ya mwezi huu wa tisa. Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania,Rosemary Lulabuka akipokea msaada huo kutoka kwa wanafunzi hao, amewapongeza na kuwaomba watanzania wengine kuwa na moyo wa kujitolea na kuchangia kampeni hii katika kuhakikisha wanafunzi wa kike wa sekondari wanafikia ndoto zao kielimu. Naye mratibu wa mabalozi wa kampeni hii Rebeca Gyumi amewaomba watanzania kwa nafasi zao kujitolea kwa chochote walichonacho kuhakikisha kuwa mradi huu unakuwa ni wa mafanikio. Michango katika kampeni hii inatolewa kwa njia mbalimbali zikiwemo kutuma neno Changia Tofali kwenda namba 15564 kwa mteja wa mtandao wa simu wa Voda na Tigo, kutuma fedha katika akaunti ya Mfuko iliyopo benki ya CRDB 01J1027639900, au kwa kupitia akaunti ya M-pesa namba 404040 Unaweza pia kuwasilisha mchango wako katika ofisi za Mamlaka ya Elimu Tanzania zilizopo Mikocheni barabara ya kambarage au katika vituo vya televisheni vya ITV, channel ten na Clouds Media Group. Katika Kampeni hii Mamlaka inalenga kujenga hosteli 30 kupitia michango ya wadau mbalimbali. Kiasi kinachohitajika mpaka kukamilika kwa mradi huu ni shilingi za kiatanzania 2.3 bilioni ambapo kila bweni litagharim shilingi millioni 78 bila samani. Jumla ya wanafunzi wa kike 1,504 watahudumiwa pindi ujenzi wa hosteli hizi utakapokamilika.

0 comments:

Post a Comment