Help Children
Love them
Saidia Watoto

Saturday, August 4, 2012

Mwasiti na Banana watoa elimu ya muziki kwa washiriki wa Epiq BSS 2012

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Tanzania House of Talent (THT) Mwasiti Almasi akiwafundisha washiriki wa shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS 2012) kuimba baadhi ya nyimbo shindano hilo litaanza kurushwa rasmi leo na limedhaminiwa na Zantel

Elimu ikiendelea
WASHIRIKI wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 waliofanikiwa kuingia hamsini bora jana walipewa elimu ya muziki kutoka kwa wasanii Banana Zorro na Mwasiti Almasi. Elimu hiyo ya muziki ilijumuisha uwezo wa kuimba, kupanga sauti, kujiamini na masuala mengine muhimu kwenye sanaa ya muziki. Wakiwa na wasanii hao washiriki wa EBSS 2012 pia walipata nafasi ya kuuliza maswali kuhusiana na maendeleo ya muziki pamoja na biashara ya muziki kwa ujumla. Akizungumzia mafunzo hayo msanii Banana Zoro alisema kuwa washiriki hao wengi wanaonekana kuwa na vipaji pamoja na uwezo wa juu wa kuimba na kuongeza kuwa elimu hiyo itawasaidia sana katika shindano hilo. “Unajua muziki ni zaidi ya kuimba, muziki unajumuisha masuala mbalimbali kama vile namna ya kuuimba wimbo, kujitengenezea muonekano wa kisanii na mengineo mengi” alisema Banana. Kwa upande wake msanii kutoka Nyumba ya sanaa Tanzania, Mwasiti Almasi, alisema kwa namna alivyowaona wasanii hawa anaamini mchuano utakuwa mkali sana mwaka huu. ‘Kwa kweli kila kijana niliyemsikiliza nimeona ana kipaji kikubwa, hali inayonifanya niamini mshindi wa mwaka huu atakuwa moto wa kuotea mbali’ alisema Mwasiti. Jumla ya wasanii 50 wapo jijini Dar es salaam kwa ajili ya kushiriki shindano hilo ambalo leo linaanza kuoneshwa rasmi katika kituo cha ITV likidhaminiwa na kampuni ya simu za mikononi ya Zantel.

0 comments:

Post a Comment