Help Children
Love them
Saidia Watoto

Wednesday, August 8, 2012

Mabalozi wa kuchangia ujenzi wa mabweni wavamia bungeni

Mh. Sophia Simba Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na Watoto akitoa mchango wake kuchangia kampeni hii bungeni. Ili kuchangia pia unaweza kutuma neno CHANGIA TOFALI kwenda namba 15564 ambapo utakatwa shilingi 250 tu za kitanzania.

Mratibu wa kampeni ya Elimu yao Jukumu letu Rebeca Gyumi akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda jinsi harambee ya uchangiaji mabweni inavyoendeshwa na makusudio ya harambee hii. TEA inakusudia kuchangisha jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 2.3 zitakazotumika kujengea hosteli 30 katika mikoa minane nchini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii na Mbunge wa viti maalumu(CCM) Mh. Margreth Sitta akitoa mchango wake kwa TEA katika kuchangia harakati za Mamlaka ya Elimu Tanzania kuhakikisha wanafunzi wa kike wanakuwa na makazi salama. Habari kamili Kikundi cha wasichana maarufu watano katika nyanja mbalimbali nchini wameungana kwa pamoja na kuamua kwa hiari kuunga mkono jitihada za Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) za kutafuta kiasi cha shilingi za kitanzania billion 2.3 zitakazotumika kujenga hosteli 30 ambazo zitahudumia wasichana wa shule za sekondari 1,504. Kikundi hicho cha mabalozi wa kampeni hii kinaundwa na Rebeca Gyumi(Mtangazaji wa kipindi cha FEMA) Faraja Nyalandu (Miss Tanzania 2004), Nancy Sumari (Miss Tanzania 2005) Jokate Mwegelo(Mshindi wa pili Miss Tanzania 2006) na Mariam Ndaba(Mwana mitindo na mmiliki wa blog) kiliguswa kwa namna ya kipekee na na jitihada za TEA na hivyo wakaamua kwa hiari kuungana na TEA katika kuhamasisha watu kujitokeza na kuchangia kampeni hii. Mabalozi hao wamefika bungeni na baada ya kutambulishwa wameendelea na zoezi la kuchangisha fedha kutoka kwawabunge wa bunge hilo.

0 comments:

Post a Comment