Help Children
Love them
Saidia Watoto

Saturday, February 16, 2013

Wazazi wawatia bakora walimu wa sekondari


Na Elimubora

WALIMU watatu wa Shule ya Msingi Misingeni mkoani Kigoma Ujiji wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao kufuatia kushambuliwa na kundi la wazazi wenye watoto kwenye shule hiyo.

Habari za uhakika zilizopatikana mjini hapa na baadaye kuthibitishwa na uongozi wa shule hiyo zinaeleza kuwa uvamizi huo wa wazazi hao unafuatia kupiga kitendo cha mwalimu mmoja wa shule hiyo kuwaadhibu watoto wao.

 Hilda Msita ambae ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, alisema kuwa chanzo cha mgogoro huo kinatokana na wazazi kupinga kitendo cha Mwalimu wa shule hiyo, Mathias Banzi  kuwaadhibu watoto wao kwa kuwachapa viboko kutokana na utovu wa nidhamu.

Alisema baada ya kutokea vitendo hivyo vya utovu wa nidhamu kwa watoto hao Mwalimu Banzi aliwachapa viboko wanafunzi hao na ndipo mwanafunzi mmoja (Fadhili Mlibo) alikimbia na kwenda kutoa taarifa kwa wazazi wake kuhusu jambo hilo.


Mwalimu Mkuu wa shule huyo, Hilda Msita aliwataja walimu waliojeruhiwa kwenye sakata hilo kuwa ni pamoja na Mathias Banzi, Barnabas Matalisi na Sikujua Bunoge ambao baada ya kipigo cha wazazi hao walitibiwa katika hospitali ya mkoa Kigoma Maweni na kuruhusiwa.


Alisema kuwa baada ya kufika nyumbani na kutoa taarifa kwa wazazi wake, Mama wa mwanafunzi huyo, Amina Rashidi aliwaeleza wazazi wengine wenye watoto shuleni hapo na ndipo kundi la wazazi zaidi ya 20 walivamia shuleni hapo wakiwa na silaha za jadi na kuwajeruhi walimu.


Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, Mohammed Kihenya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba polisi inamshikilia Amina Rashidi mzazi wa mmoja wa watoto walioadhibiwa katika sakata hilo.

Kamanda Kihenya alisema kuwa pamoja na kumshikilia mzazi huyo kwa kufanya vurugu mahala pa kazi na kujeruhi pia inawatafuta watu wengine ambao walihusika katika vurugu hizo.


0 comments:

Post a Comment