Help Children
Love them
Saidia Watoto

Friday, February 1, 2013

Sakata la hali ya elimu na mtaala linazidi kushika moto Dodoma

Mbunge wa kuteuliwa  kwa tiketi ya NCCR Mageuzi  James Mbatia amesema kuwa kuna kila dalili ya harufu ya rushwa na ufisadi katika utoaji wa tenda za uchapishaji wa vitabu vya ziada na kiada. 






Mbatia alisema hayo jana wakati akiwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusiana na mitaala na hali ya elimu nchini.

Alisema kuwa hali inaonesha kuwa Taifa linakuwa kwenye mgogoro mkubwa katika sekta ya elimu ambapo alisema kuwa mamlaka husika zimeshindwa kufanya kazi zake.

Pia alikataa kufunga hoja kuhusiana na suala la mtaala wa elimu kuwa una matatizo ambapo alimwelezea Naibu Spika wa bunge hilo kuwa hawezi kuacha kuzungumzia suala la mtaala kwa kuwa  hali ya elimu ni mbaya sana mkoani humo

0 comments:

Post a Comment