Help Children
Love them
Saidia Watoto

Friday, February 15, 2013

Elimu gani tena itolewe kupambana na wauaji wa walemavu wa ngozi?



 

WATU watatu  wakazi  wa kitongoji cha Mkoe  kijijini Miangalua  wilayani
Sumbawanga wamekamatwa na kuhojiwa na Polisi Mkoa wa Rukwa wakituhumiwa
 kuhusika  na kisa  cha kumnyofoa  mlemavu wa ngozi , Maria Chambanenge
 (39) na kutokomea nao .

Akizungumza na mwandishi wa habari  hizi  jana katika kitongoji  hicho  cha
Mkoe kijijini Miangalua , Diwani wa Kata  ya Miangalua , Semakweli Sindani
 amethibitisha  kukamatwa kwa  watuhumiwa hao  ambapo  amewataja  wawili
 kati yao  akiwemo  mume  wa  mwanamke  huyo mlemavu  wa ngozi  aitwaye
Gabriel Yohana (43) na  mdogo wake  Gaudensi  Yohana .

Hata hivyo diwani  huo  hakuweza kutoa  taarifa zaidi  huku akieleza kuwa
 watuhumiwa  hao  ni miongoni  mwa genge  la majambazi  ambao  kabla ya
kumtendea  unyama huo  mwanamke  huyo albino siku chache kabla wanadaiwa
 kuvamia  nyumba  moja  kijijini Ilamba , Kata ya Kipeta wilayani  humo
ambapo  walimteka  kijana mmoja mlemavu  wa ngozi  ambaye jina  lake
 halikuweza kufahamika  mara moja ambapo  ‘kimuujiza’  alifanikiwa
kuwaponyoka  na kurejea kijijini humo.

Hata  hivyo  wake wenza wa Maria waitwao Honoratha  Xevia  maarufu mama
Daria na mwenzake Estha Pesambili  maarufu kama mama Ray wamedai  mgeni
 aliyefikia  nyumbani kwao  na kuishi hapo  waliyemtaja kwa jina moja  la
Sirukala  kuwa amekamatwa….

Wakimweleza  mwandishi wa habari  hizi  walidai kuwa  wao  wanafahamu  kuwa
mume  wao Gabriel  yupo mjini  akimuuguza mke mwenzao Maria  ambaye  bado
 amelazwa  katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga

“Huyu  mgeni , Sirukala  yeye tulikuwa  tukiishi  naye  nyumbani  akisaidia
kupalilia  mashamba yetu hapa  siku  hiyo  ya tukio  saa 10 jioni aliondoka
 nyumbani  hapa  bila ya kutuaga hadi leo  bado  hajarudi  hadi tulipopata
 taarifa kuwa amekatwa  akihojiwa na pilisi mjini Sumbawanga .

Sisi  tunachofahamu ni  kwamba  mume  wetu  bado  yupo  hospitalini  mjini
Sumbawanga  akimuuguza mke mwenzetu ambaye amelazwa huku …alisema mama  Ray
.

Habari ambazo pia zimethibitishwa na baadhi ya wakazi wa kitongoji hicho
cha Mkoe kijijini Miangalua akiwemo Diwani wa Kata hiyo ya Miangalua (CCM)
, Sindani.

Hata hivyo habari za kipolisi licha ya kukiri kukamatwa kwa watuhumiwa hao
watatu lakini  mtoaji  taarifa wake  amekataa  kutaja majina yao kwa
 kigezo kuwa bado upelelezi  unaendelea  ili  kuwabaini  wengine  “Ofisa wa
Upelelezi  wa Mkoa wa Rukwa , (Peter Ngusa)  bado yuko eneo  la tukio
 akiongoza msako  huko ….. kwanza wewe  nani  kakupatia habari  hizi  akiwa
tayari atakutaarifu  kwa sasa ni mapema mno “ alisema mtoa habari wa polisi
 kwa masharti ya kutoandikwa jina  lake gazetini.

Hata hivyi  jitihada  za  mwandishi wa habari  hizi  kumpata Ngusa  katika
 simu yake ya mkononi  ziligonga  ukuta kwani  ilikuwa  haipatikani .



Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga , Mathew  Sadoyeka  akiongozana  na  wajumbe
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama  wa  wilaya  hiyo  kutembelea  nyumba
 alimofanyiwa  unyama  huo  Maria  katika kitongoji  cha Mkoe  alielezwa
 na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Luka  Mwampamba kwamba  mama huyo alifanyiwa
 unyama huo  huku mtoto wake mkubwa  wa kike  aitwaye Shukuru  (7)
anayesoma  Darasa la Kwanza akishuhudia .

Inadaiwa  mama  huyo  mlemavu  wa ngozi  ambaye  ana watoto  wanne  wote
 si  albino alikuwa akimnyonyesha mtoto wake  mchanga  wa miezi  miwili .


Akizungumzia tukio hilo juzi , Gabriel  ambaye ni  mume wa Maria  wakati
akimuuguza mkewe huyo katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini hapa ambapo
amelazwa  kwa matibabu  alidai watu hao wakiwa hawafahamiki idadi,
walivamia nyumba yao usiku wa manane wakati mkewe akiwa amelala na watoto.
Alidai kuwa kabla ya kufanya unyama huo, watu hao walifunga milango ya
nyumba zote kijijini hapo kwa kamba.

Kwa mujibu wa madai ya Gabriel, Mariamu ni mkewe mdogo, ana watoto wanne na
usiku wa tukio, alikuwa amelala kwa mke mkubwa aitwaye Honoratha .

Alidai kuwa baada ya wavamizi hao kufanya unyama huo, mtoto mdogo wa kaka
yake, alimwamsha akimwambia kusikia kelele kutoka nyumba ya mke mdogo.

“Ndipo nilipokurupuka kwenda huko, lakini nilikuta milango yote imefungwa
kwa nje kwa kamba ya katani na dirisha limevunjwa na watoto na mama yao
wakiwa wanalia.

“Tulipofungua mlango na kuingia ndani, nilimkuta mke wangu akiwa
anagaragara sakafuni kwenye dimbwi la damu kwa maumivu, huku mkono wake wa
kushoto ukiwa umekatwa na watu wasiofahamika na kutokomea nao
kusikojulikana,“ alisema.

Gabriel, ambaye alimsindikiza mkewe hadi hospitali ya mkoa wa Rukwa mjini
Sumbawanga ambapo amelazwa kwa matibabu, alidai kuwa kabla ya kumfikisha
hapo, mkewe huyo alipewa huduma ya kwanza katika zahanati katika mji mdogo
wa Laela, wilayani Sumbawanga.

Alisema walilazimika kupata huduma ya kwanza kwa kuwa Maria alikuwa na
majeraha makubwa kichwani, baada ya kukatwa na panga na watu hao
wasiofahamika.

Habari za kipolisi  zimeleza kuwa  watuhumiwa  hao  watafikishwa mahakamani
 mara tu upelelezi wa  awali wsa shauri  lao utakapo kamilika  huku msako
 mkali ukiendelea kuwabaini  wengine  ambao  wanadai walifanikiwa kutoroka
na kujificha kusikojulikana .
wakati huohuo, MKAZI  wa kijiji cha Miangalua  wilayani Sumbawanga  , Bernad  Chambanenge
 (79)  ambaye  ni  baba mzazi  wa mwanamke  mwenye ulemavu wa ngozi, Maria
Chambanenge (39), mkazi wa kitongoji cha  Mkoe amelaaani  na kusikitishwa
 na unyama  aliofanyiwa  binti yake  huyo kwa kunyofolewa mkono  wake wa
kushoto  na watu wasiofahamika kisha kutokomea  nao .

A kiwa na uso  wa huzuni  huku  kijijini Miangalua  jana  alimweleza
 mwandishi  wa  habari  hizi kuwa    kisa hicho  cha kikatili
 alichofanyiwa  binti yake  huyo  hivi karibuni  kimewatia  hofu kubwa
 wanawe  wengine  ambao  nao  pia  ni  walemavu  wa  ngozi  wanaoishi
 kijijini  humo .

Kwa mujibu wake  mkewe aitwaye Ezenia Mtavya (70) amemzaliwa watoto 12
 ambapo  sita miongoni mwao   ni  walemavu  wa  ngozi  miongoni mwao  walio
hai  kwa  sasa ni wanne  baada ya wawili  kufariki  dunia .

“Mie  na mke wangu hatujawahi kuwanyanyapaa  watoto hawa  ambao  ni  albino
 kwani wote  tumewalelea  sawa sawa bila  ubaguzi  wa aina  yeyote
 isitoshe Maria  ni kipenzi  changu …….. kwa  sasa  naishi  na
 kitindamimba  aitwaye  Zaina  ambaye   pia  ni albino



Hivyo  kutokana  na  usalama wa wanangu hawa  kuwa  hatarini  naomba
Serikali  iwapatie  ulinzi  wa kutosha” alisema

Akisimulia  kisa cha binti yake huyo  kunyofolewz mkono  wake wa kushoto
 alidai  kuwa usiku  huo  wa mananbe akiwa amelala  nyumbani  kwake  katika
kitongoji  cha Mkoe  kijijini Miangalua  na  watoto  wake wawili  ambao  si
 albino  akiwa anamnyoyesha  mtoto wake  wa miezi  miwili  watu
wasiofahamika  waliingia  ndani ya nyumba hiyo wakipitia dirishani  na
 kumyofoa mkono  wake wa kushoto  wakitumia panga .

Alidai kuwa  wakati unyama  huo  ukifanyika,  mtoto  wa  mlemavu huyo  wa
ngozi  wa kike mwenye umri wa miaka  saba  anayesoma  Darasa la Kwanza ,
aitwaye  Shukuru aliyekuwa amelala chumbani na mama yake  alishuhudia
majambazi  hao walikuwa na  panga  wakiushika  mkono  huo wa kushoto wa
mama yake  baada ya kumlaza mama  yao  sakafuni  kisha  wakaukata  na panga
 na kutokomea nao .

Hata hivyo baba  huyo  mzazi  amedai  mume  aliyemuoa  binti yake  huyo
 aitwaye Gabriel Yohana (43),  kuwa  ni  mwanaume katili  kwa kumtuhumu
 kumpiga mara kwa mara mkewe huyo   bila ya sababu za msingi  na
kumsababishia makovu mwili .Gabriel ana  wake watatu  ambao  wote  kwa
pamoja  wamemzalia watoto 11 wote si albino.

Wakizungumzia mkasa huo  wake wenza  wa Maria  akiwemo  bi mkubwa  aitwaye
 Honoratha Xavier  mama wa watoto  sita  amedai kuwa  usiku  huo wa tukio
 akiwa  chumbani  na mume wao Gabriel  ghafla  aligutushwa na sauti kali
 ambayo alidhani  ni mlio wa fisi  ambapo  alimwamsha mumewe ambaye
alichukua upinde na mshale  na kutoka nje .

“Ndipo  baadaye  tulipata taarifa  kuwa mwenzetu  Maria  ameumizwa na
 majambazi  walimvamia nyumbani kwake “ alisema .

Huku Esta Pesambili mama  ya mtoto mmoja ambaye ni mke wa pili  wa Gabriel
 alidai kuwa  yeye  binafsi  hwakuwa  na masikilizano na Maria  kwa kuwa
ana wivu sana  ambapo  alikumbuka  katika mkasa mmoja  wakati  wake  wote
 watatu wakishi  katika nyumba moja  katika kitongoji  hicho  cha Mkoe
 ambapo  waligombana na  Maria alijeruhi  titi lake  la kulia  kwa jembe .

“Ndipo  kutokana na   kutoelewana kwetu  Gabriel  aliamua  kumjengea
 nyumba  yake peke yake  Maria  na kumwamishia  huko  ndipo ukawa mwisho
 wa  ugomvi  wetu …. Licha  ya kutoelewana kwetu  hakika nimesikitishwa
 sana  na  unyama  aliofanyiwa na  mwanamke mwenzetu” alisema kwa uchungu.

Kwa upande wake Zaina  kitindamimba wa mzee Chamanenge ambaye pia  ni
albino  amedai licha  ya kuwa  na huzuni  kubwa  kwa unyama  aliofanyiwa
dada yake   mbali ya kuwa  ni mwanamke lakini pia ni albino mwenzake
 lakini  moyoni alifurahia  kusafiri  hadi  Sumbawanga mjini  kumwona dada
yake huyo  ambaye bado  amelazwa  katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa
akipatiwa  matibabu.

“Sijawahi  tangu nizaliwe miaka 20  iliyopita  kusafiri  umbali huu tena
kwa gari  hii  ni mara yangu ya kwanza  ndio maana nimetapika  njia nzima
 sijawahi kusafiri kwa  gari  lakini  baahati mbaya   furaha yangu  hii
 imegubikwa na majonzi na huzuni  kubwa moyoni “ alisema huku akibubujikwa
na machozi.

0 comments:

Post a Comment