Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, July 15, 2012

Majaji EBSS waendeleza elimu ya muziki kwa washiriki wa EBSS

 Jaji Master Jay akitoa elimu kwa mmoja kati ya washiriki waliojitokeza katika usaili wa Mwanza
Mshiriki akiwa anasikilizia elimu hiyo mara baada ya kumaliza kuimba na kuambiwa kuwa alichemka.



Na Mdau wa elimuboratanzania, Mwanza.
VIJANA wa mkoa wa Mwanza wameelezea kufurahishwa kwao na elimu ya bure iliyotolewa na majaji wa EBSS mkoani Mwanza ambapo waliahidi kufanyia kazi elimu hiyo.

Elimu hiyo ni kuhusiana na namna ambavyo wanaweza kujifunza kupandisha sauti zao, kupanga vina na kuimba aina zote za sauti.

Wakati huohuo katika hali isiyokuwa ya kawaida wakazi  wa  mkoa wa Mwanza juzi walijitokeza kwa wingi katika usaili wa shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS) mkoani hapa hali iliyosababisha wengi wao kukosa  nafasi ya kuimba na kulazimika kurudi tena jana.

Katika usaili huo uliofanyikia katika uwanja wa CCM Kirumba ulihudhuriwa kwa mamia ya wasichana na wavulana huku wengine wakiwa wamebeba  vifaa mbalimbali vya muziki kuashiria kuwa wanaifahamu vema fani hiyo.

Zoezi la kuimba lilianza majira ya saa mbii asubuhi ambapo majaji walianza kusikiliza vipaji hivyo na ilipofika majira ya saa kumi na moja jioni bado kulikuwa na watu wengi waliokuwa bado wanahitaji nafasi ya kuendelea kuimba.

Kutokana na muda kuwa umeenda walilazimika kuambiwa kurudia tena jana huku wengi baadhi yao walikuwa wamefanya siku ya kwanza vema waliitwa tena kuimba kwa mara ya pili ili kuchaguliwa.

Mmoja kati ya wafanyakazi wa kampuni ya Benchmark  Production inayoandaa shindano hilo alisikika akisema kuwa hali hiyo haijawahi kutokea kwa mkoa wa Mwanza kwa kuwa watu wamekuwa wakijitokeza kila mwaka lakini sio kwa idadi hiyo.

Mkoa wa Mwanza ambao mwaka juzi ulitoa mshindi wa shindano hilo Paschal Casian umekuwa na hamasa kubwa ya wakazi wake kujitokeza kwa wingi kushiriki katika shindano hili kubwa na la aina yake linalodhamiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zantel.

1 comments: