Help Children
Love them
Saidia Watoto

Friday, May 11, 2012

Wanafunzi jitokezeni kEsho katika Ukumbi wa Nkurumah UDSM


 Meneja Masoko wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Omari Mbura akitoa maelezo kwa waandishi kuhusiana na tukio hilo la kesho katika ukumbi wa Nkuruma, pembeni yake ni Mustapha Hasanali
Mtaalamu kutoka nchini India ambae ni mmoja kati ya waratibu wa shughuli hiyo ya kesho.


Na Mwandishi wa Elimubora
WASANII wa muziki wa kizazi kipya Dully Sykes na Chidi Benz watasindikiza uzinduzi shindano la wanafunzi litakalofanyika kesho katika Ukumbi wa Nkuruma uliopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Shindano hilo litakalozinduliwa kesho linashirikisha wanafunzi wa vyuo vikuu nchini chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ushirikiano na mpango wa kuendeleza wajasiriamali vijana unaodhaminiwa na serikali ya India kupitia mradi wake wa IndiAfrika.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Meneja Masoko wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Mbura Omari alisema kuwa hakutakuwa na kiingilio siku hiyo ya kesho ambapo shughuli itaanza tangia asubuhi.

Akizungumzia shindano hilo Mbura alisema kuna vipengele vingi ambavyo vijana wanashindanishiwa ikiwa mojawapo ni kuangalia uelewa wao katika Nyanja za biashara, mazingira, uchumi na nyinginezo nyingi.

Alisisitiza kuwa utamaduni ikiwa ni moja kati ya Nyanja muhimu wanafunzi wanatakiwa kuandika masuala muhimu ya kujadili katika Nyanja ya utamaduni.

Alisema kuwa ili kuweza kuibuka mshindi katika shindano la hapa nchini na lile la Afrika kiujumla wanafunzi wanatakiwa kuonesha umakini katika kutetea kile ambacho wanaona kuwa kinafaa katika masuala ya utamaduni.

Alisema kuwa mshindi wa jumla katika kanda ya Afrika atapata milioni kumi lakini pia kutakuwa na mshindi wa nchi ambapo atapatikana mmoja katika kila Nyanja.

“ Katika shindano hili vijana watashirikiana katika nyanja za uandishi wa insha, upigaji wa picha na ubunifu katika kuwasilisha ujumbe pia lakini pia wataandika michanganuo yao katika Nyanja mbalimbali ambapo lengo ni kuwapatia fursa ya kuonesha uwezo wao katika kufikiri” alisema Mbura.

Katika kusisitiza na kuonesha nia ya kuimarisha ushirikiano huo mbunifu wa mavazi nchini Mustapha Hasanali aliahidi kusaidia mbunifu chipukizi mmoja katika wiki ya mitindo ya Swahili ambapo ataenda kushiriki kuonesha mitindo nchini Afrika Kusini.
Mwisho

0 comments:

Post a Comment