Help Children
Love them
Saidia Watoto

Friday, May 11, 2012

BSS NA BASATA WAPEANA SOMO

 Msanii wa muziki wa asili Chemundu Gwao akiwa na wasanii waliofanya vema katika BSS mwaka jana Haji Ramadhan na Wazzi
 Chemundu Gwao akichangia mada
Mmiliki wa Bernchmark Production ambae ndio mmiliki wa program ya BSS Ritha Paulsen  akisistiza jambo kwa mratibu wa BSS katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Vicky Temu.


Na Evance Ng’ingo
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wasanii waliotoka katika mradi wa Bongo Star Search kuwa na mikakati ya kujiendeleza wenyewe badala ya kutegemea kusaidiwa na mradi huo pindi shindano linapokwisha.

Wito huo ulitolewa jana na mratibu wa BSS katika Basata Vicky Temu wakati akichangia mada katika mkutano uliowashirikisha BSS na wadau wa sanaa na kufanyika Basata.

Vicky alisema kuwa wasanii hao wanatakiwa kutambua kuwa uhusiano kati ya BSS na wasanii hao unamalizika mara baada ya shindano hivyo wanatakiwa kutumia vema elimu ya muziki waliyoipata wakiwa ndani ya shindano hilo kujiendeleza zaidi.

Hata hivyo alimtaka mwandaaji wa shindano hilo Ritha Paulsen kuwaendeleza wasanii hao ikiwa pamoja na kuingia mkataba na studio za kurekodia muziki kwa lengo la kuwaendeleza zaidi watakaofanya vema pindi shindano linapomalizika.


Wakati huo huo mwandaaji wa shindano hilo Rita, aliwataka waandishi pamoja na watangazaji wa redio na luninga kuwasaidia wasanii watokao katika BSS badala ya kuwakatisha tama.

Alisema kuwa kuna wadau mbalimbali katika vyombo vya habari na sanaa kiujumla ambapo wanawakatisha tamaa wasanii watokanao na mradi wa BSS kwa kutotaka kuwasaidia kuwatangaza.

Katika hatua nyingine gazeti hili lilishuhudia hali ya mtafaruku katika ya Rita na BSS katika suala la upatikanaji wa kibali cha mwaka huu na suala la upangaji wa majaji.

Rita alilalamikia kitendo cha Basata kutaka kumpatia kibali cha muda cha kuandaa shindano hilo kwa mwaka huu mpaka pale atakapomweka bayana mdhamini wake wa mwaka huu huku Rita akisisitiza kuwa apewe kibali kamili ili mdhamini wake aweze kusaini mkataba kwa kuwandio atakuwa na imani kuwa shindano lipo.

“ Sasa mkinipa kibali kamili si ndio mdhamini atatoa huo udhamini na kutuhakikishia kuwa anatudhamini kwa mwaka huu au? Mkinipa kibali cha kawaida ntashindwa kupata udhamini kwa nini kwanza msinipe kibali cha mwaka mzima” alihoji Rita.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Kitengo cha Matukio cha Basata, Malimu Mashili alisema kuwa baraza hilo haliwezi kutoa kibali kamili kabla halijapata mwelekeo wa shindano la mwaka huu ili kwa kuwa chochote kikiharibika ni baraza ndio litahusika.

Kikao kilimalizika huku Basata ikiwa imemtaka Rita kuwasilisha bajeti inayotaja zawadi, na gharama nyinginezo licha ya kuwa Rita aliwataka wampatie kibali kamili ili aweze kusaini mkataba na mdhamini wake lakini hata hivyo alisema kuwa suala la kutaja zawadi ni mapema mno kwa kuwa wadhamini wengine hujitokeza shindano likiwa limenza.

Mtafaruku mwingine uliibuka katika suala la upatikanaji wa majaji wa shindano hilo ambapo Basata ilimtaka Rita kuwapelekea majina ya watu watano ili iweze kuwachagua watatu kati yao huku ikisisitiza kuwa huo ni utaratibu wa kawaida.

Akionesha kushangazwa na utaratibu huo Rita alisema kuwa anapenda kuwatumia majaji wake wale wale kwa kuwa ndio ameshawajengea hisiza nzuri kwa washabiki wa BSS na huvuti kipindi hivyo kuwabadilisha sio haki.

Mkutano huo ulivuta hisia za wadau  mbalimbali wa sanaa waliokuwa katika mkutano huo uliodumu kwa saa tatu kwa lengo la kutathmini maendeleo ya BSS, lakini hata hivyo Basata ilimpongeza kwa kuendesha shindano hilo kwa miaka sita bila ya kusimama.
Mwisho 

0 comments:

Post a Comment