Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, June 24, 2012

Zantel yanogesha Epiq Bongo Star Search Zanzibar

 Huyu kijana alikuwa ni mmoja kati ya waliwakuna majaji
 Mkuu wa Mawasiliano wa kampuni ya simu ya Zantel Awaichi Mawala (kushoto) akiimba na wasanii waliokuwa wakisubiria kuitwa ndani kwenye kuimba
Kundi kubwa la watu wakisubiria
                                      
Majaji wakifuatilia shindano hilo ambapo pia walitoa somo la muziki


Na Mwandishi Wetu
UWANJA wa burudani uliopo katika eneo la Ngome Kongwe jana ulifurika maelfu ya vijana waliojitokeza kushiriki katika kinyang’anyiro cha kuchaguliwa kuingia katika fainali za shindano la Epiq Bongo Star Search 2012.

Huku kukiwa na idadi kubwa ya washiriki wasichana pia kulikuwa na washiriki ambao waliwasili wakiwa na vifaa mbalimbali vya kupigia muziki kama vile gitaa,vinanda na vinginevyo ikiwa ni mikakati yao ya kujihakikishia kuchaguliwa.

Akizungumzia usaili wa Zanzibar Jaji Mkuu wa EBSS 2012 Ritha Paulsen alisema kuwa ameguswa na mwamko wa washiriki kutoka Zanzibar.

‘Zanzibar ina vijana wengi wenye vipaji na ambao wanatakiwa kuendelezwa ili kufikia malengo yao katika muziki’ aliongeza Ritha.

Alisema kuwa kupitia shindano la EBSS ambalo linadhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi Zantel anatarajia kupata vipaji vingi katika mikoa yote ambayo usaili unaendelea.

Naye Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel kwa Zanzibar Mohamed Mussa mbali na kufurahishwa na idadi kubwa ya washiriki waliojitokeza aliwataka vijana wa kisiwani hapa kutambua kuwa muziki unaweza kuwapatia ajira kubwa.
‘Muziki ni ajira, na ndio maana sisi Zantel tumeamua kuwekeza kwenye mashindano haya ili kuwapa fursa vijana wengi zaidi’ alisisitiza bwana Mussa.




0 comments:

Post a Comment