Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, June 10, 2012

Wazir wa Fedha na Uchumi atoa somo kwa wachumi Tanzania


Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Fedha na Uchumi William Mgimwa amesema kuwa wataalamu katika sekta ya fedha wanatakiwa kujiamini na kuwa na mikakati endelevu kwa lengo la kukuza na kuinua uchumi wa nchi.

Mgimwa alisema hayo hivi karibuni wakati akizingua matawi mawili ya benki ya Ecobank yaliyopo Quality Mall na Mwenge ambapo alisifia uzinduzi wa matawi hayo mapya kwa kusisitiza kuwa huo ni ushahidi wa kuwa na wafanyakazi wenye kujiamini na kuwa na nia na maendeleo.

Alisema kuwa iwapo wachumi wa kiafrika wakijiamini wataiwezesha sekta binafsi kuunganisha uchumi bora kwa manufaa ya watanzania na waafrika kiujumla.

“Kwa  benki inayomilikiwa na Waafrika, kusimamiwa na Waafrika, kwa ajili ya kuhudumia kwa Waafrika na wafanyabiashara wa Afrika, kukua ndani ya miaka 25 tu na kuwa taasisi ya fedha yenye daraja la dunia na sifa za kimataifa, ni kweli inastahili pongezi.” Alisema Mgimwa.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ecobank Tanzania Limited Peter Machunde alisema kuwa benki hiyo tayari ina  matawi matano katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam, ina mpango wa kufungua tawi jingine Arusha na Mwanza kabla ya mwisho wa mwaka 2012.

Alisema kuwa benki hiyo inalenga kuboresha uchumi wa nchi kwa kutoa bidhaa na huduma kulingana na nguvu na uongezekaji wa mahitaji ya wateja.

Mwisho

0 comments:

Post a Comment