Help Children
Love them
Saidia Watoto

Monday, June 18, 2012

Zantel kupitia Epic Bongo Star Search yafanikisha elimu ya muziki kwa wasanii chipukizi

 Mkurugenzi wa Benchmark Production akimpokea mtoto mshiriki huyu aliyefahamika kwa jina la Joha
 Mkuu wa Mawasiliano wa Zantel Awaichi Mawalla akitoa damu kuchangia kituo cha damu cha Dodoma, pia alitoa elimu na kuwasihi vijana kujitokeza kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu wenye mahitaji ya damu
 Mshiriki huyu ni mwanafunzi wa kidato cha sita na alijitaidia kuonesha uwezo wake ingawaje hakufikia kiwango na majaji walimpatia elimu ya muziki na kumtaka afanye vema
Hawa walipongezana kwa hatua waliyofikia ingawaje hawakupita lakini walinufaika na elimu ya muziki siku hiyo.


Na Mwandishi wa Elimubora Dodoma
PAZIA la shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS) kwa mkoa wa Dodoma limefungwa rasmi huku vipaji kibao vikiwa vimejitokeza na kuwavutia majaji.

Kilichovutia zaidi ni washiriki wa miaka 16 ambao walionekana kuimba vema na kuwa kivutio hata kwa washiriki wenzao waliofurika katika ukumbi wa Royal Village.

Akizungumzia shindano hilo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Benchmark Production inayoandaa shindano hilo Ritha Paulsen alisema kuwa amevutiwa na wingi wa washiriki mkoani hapa hasa idadi ya washiriki wasichana pia.

Alisema kuwa ikiwa ni mara ya kwanza kuruhusu washiriki wa miaka 16 kuingia katika usaili wa EBSS 2012 ameshuhudia hazina kubwa ya vipaji  vya washiriki wa umri huo.

Katika usaili huo kulikuwa na washiriki wa aina mbalimbali wakiwamo wanafunzi, wafanyabiashara ndogondogo, vijana wa mitaani na wadau wengineo wa muziki.

Kwa kuthamini umuhimu wa akina mama na watoto mshiriki aliefika kuonesha kipaji chake katika ukumbi huo alipewa nafasi ya kuimba ili aweze kuwahi kuondoka.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Zantel ambao ni wadhamini wakuu wa EBSS 2012  Awaichi Mawalla mbali na kuvutiwa na ushiriki wa vijana waliojitokeza pia alihamasisha upimaji wa damu kwa kuchangia damu kwa kituo cha damu mkoani Dodoma.

“ Kwa kupitia EBSS 2012 tunataka kuwafikia vijana sio tu katika muziki bali pia hata katika kuhamasisha masuala mbalimbali yahusuyo jamii kama vile hili la kuchangia damu na mengineo” alisema Awaichi.

Washindi watakaopatikana watatangazwa baadae katika vyombo vya habari. Baada ya Dodoma kwa sasa inafuata Zanzibar ijumaa ijayo katika eneo la Ngome Kongwe.
Mwisho


0 comments:

Post a Comment