Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, June 10, 2012

REPOA na ESRF watoa somo la bajeti kwa kamati za bunge

 Mkurugenzi Mkuu wa Economic and Social Research Foundation, Bohela Lunogelo
 Mtafiti kutoka Taasisi ya Research on Poverty Alleviation (REPOA) Jamal Msami akichangia mada
 Mwenyekiti wa kamati ya hesabu za serikali John Cheyo ambae pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi akizungumza na ofisa habari wa Repoa Hannah Mwandolwa
Mbunge wa Kilwa Kaskazini Murtaza Mangungu(kushoto) mtafiti kutoka Repoa Msami (katikati) na Kongi Lugola Mbunge wa CCM jimbo la Mwigora.

 
Na Mwandishi wa Elimu Bora
SERIKALI imetakiwa kuvitumia vema vyanzo mbalimbali vya mapato ili kuongeza pato la taifa kutokana na ukusanyaji wa kodi katika vyanzo hivyo.

Rai hiyo ilitolewa juzi na mtafiti kutoka Shirika la Utafiti wa Kuondoa Umaskini (Repoa) Jamal Msami wakati akitoa mada katika semina ihusuyo maandalizi ya bajeti iliyoshirikisha kamati ya bunge ya hesabu za serikali.

Msami alisema kuwa serikali inashindwa kuchangia asilimia kubwa katika bajeti yake ya mwaka kwa kukosa fedha huku ikipoteza asilimia kubwa ya mapato kwa kushindwa kukusanya kikamilifu kodi.

“ Serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa inafanya utafiti na kugundua vyanzo vipya vya mapato ambavyo vinaweza kutozwa kodi badala ya kung’ang’ania vyanzo hivyo vilivyopo kila siku huku bado havitoi pato la uhakika” alisema Msami.

Pia alisema kuwa wananchi wanatakiwa  kushirikishwa kikamilifu katika upangaji wa bajeti hiyo ili kushirikisha maoni yao katika bajeti na pia aliwataka wabunge kufuatilia upangwaji wa matumizi ya fedha katika bajeti  hiyo na kujua itakavyowanufaisha wananchi.

Naye Mbunge wa Kilwa Kaskazini Kongi Mangungu alitaka kuongezwa kwa  muda wa kujadili bajeti hiyo kabla ya kuanza kwa kikao cha bunge akisisitiza kuwa muda wa wiki mbili wanaopewa hautoshi.
Pia aliishauri serikali kuweka mkakati utakaosaidia watu kutoka mikoa ya mbali kwenda mijini kutafuta huduma za mbalimbali kwa kuwa asilimia kubwa ya mzunguko wa hela unaamia katika miji hiyo.

Aliongeza kuwa serikali inatakiwa kupunguza misamaha ya kodi inayotoa kwa wawekezaji kwa kuwa inaikosesha serikali fedha ambazo zingesaidia katika bajeti yake.

Bunge la bajeti linaanza kesho huku bajeti ya mwaka huu ikiwa ni trilioni 13 na serikali ikiwa imechangia silimia 40 ya fedha hizo.

.

0 comments:

Post a Comment