Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, February 1, 2015

Kipindi cha elimu cha Hatua Jithamini chazinduliwa rasmi

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mawasiliano ya Abel and Fernandez akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Uzuri kuhusiana na kipindi hicho

Mazungumzo yakiendelea

                                          Meneja Masoko wa Cowbell Milk inayodhamini kipindi hicho cha  Luninga, Bertin Mushi
Watoto wakipanga foleni kwenda kujipatia chai ya maziwa ya Cowbell


Watoto wakipata kifungua kinywa kabla ya kuoneshwa kwa kipindi hicho

Watoto wakiangalia kipindi hicho katika ukumbi wa Cinema wa Free Market uliopo Oyster bay

Me pia nikapata wasaha wa kuangalia kipindi hicho ikiwa ni cha kwanza na kitaanza kuoneshwa katika Luninga ya Star Tv na Tv One

Hakika watoto walifurahia kipindi hicho


Fatma na Bertin wakiwa na watoto



Bertin na mwanawe katika picha ya pamoja
Na Evance Ng'ingo
KAMPUNI ya Mawasiliano ya Abel and Fernandez juzi ilizindua kipindi cha Luninga kiitwacho Hatua Jithamini kitakachokuwa kikirushwa na Luninga za Star Tv na Tv One.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya uzinduzi wa kipindi hicho uliofanyikia katika Ukumbi wa Cinema wa Free Market, Oysterbay, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Fatma Fernandez alisema kuwa kipindi hicho kinalenga kuainisha kero, vikwazo na kutoa changamoto kwa mustakabali wa elimu ya Tanzania.

Alisema kuwa kitakuwa ni kipindi chenye kutoa nafasi kwa watu mbalimbali kuzungumzia masuala mbalimbali ya elimu na tayari wamekwisha tembelea mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Tabora, Mwanza, Dodoma, Morogoro, Iringa, Songea na Mtwara kuzungumza na wananchi kuhusiana na changamoto za elimu.

Alisema kuwa kipindi hicho cha dakika 30 kitakuwa kikirushwa kila Jumamosi na Jumapili na kuwataka watanzania kufuatilia ili kutoa mawazo yao kuhusiana na nini kifanyike katika kuzikabili changamoto za elimu nchini

"Kwa hapa nchini, matokeo ya mtihani wa darasa la saba kwa mwaka jana yametoa ishara ya kuimarika elimu yetu huku ufaulu ukiongezeka kwa asilimia 6. Lakini, licha ya ongezeko la ufaulu huo bado wanafunzi waliopata alama dhaifu walikuwa zaidi ya asilimia 43 ya wanafunzi wote. Hili ni moja ya changamoto ambazo nadhani tunapaswa kuifanyia kazi kwa nguvu zote" alisema Fatma.

Aliongeza kuwa "sekta ya elimu hapa nchini, kama zilivyo sekta nyingine inakabiliwa na changamoto nyingi sana lakini ni Imani yangu kuwa tukishirikiana kwa pamoja na tukiwa na mikakati iliyo bora, changamoto hizi hazitakuwa kikwazo cha ustawi wa elimu yetu".

Kwa upande Meneja Masoko wa Cowbell Milk inayodhamini kipindi hicho cha Luninga, Bertin Mushi alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa elimu hasa ya msingi nchini Cowbell imeamua kudhamini kipindi hicho kwa kuwa nao wanasaidia elimu kwa kuwajengea afya watoto kupitia maziwa yao ya Cowbell.
==============

0 comments:

Post a Comment