Help Children
Love them
Saidia Watoto

Tuesday, November 3, 2015

Mdau wa Mitindo Deo atoa somo kwa models wa Black fox


 

Na Mwandishi Wetu
VIJANA wanaojifunza fani ya Uanamitindo hapa nchini wametakiwa kutumia muda wao mwingi kujifunza fani hiyo kutoka kwa wanamitindo wenzao wa nje ya nchi.

Wito huo ulitolewa juzi na mdau wa fani hiyo ambae ni mtangazaji wa kipindi cha Nirvana kinachorushwa na kituo cha Luninga cha East Afrika, Deogratius Chitama wakati akizungumza na vijana wanaojifunza fani hiyo.

Deo alisema kuwa kutokana na ugeni wa fani hiyo hapa nchini vijana wanaotakiwa kujiajili katika fani hiyo wanayo kila sababu ya kuwafuatilia wanamitindo wakubwa wa nje ya nchi kwa kuwa wao wameshaendelea.

Alisema kuwa kwa kufanya hivyo itawaongezea hamasa kubwa katika kujua mengi kuhusiana na fani hiyo kuanzia uendeshwaji wake hadi fursa zilizopo katika fani hiyo.

"Ukweli ni kwamba kwa hapa kwetu hii ni moja kati ya fani mpya kabisa kwa kuwa kwanza watu wengi bado wanadhani kazi kubwa ya uanamitindo ni kuonesha mavazi tu ila kuna mengi zaidi ya hapo" alisema Deo.

Aliongeza kuwa " kwa upande mwengine hii ni fani ambayo mtu unaweza kuitumia vema ukajikuta unapata kazi za kufanya matangazo ya biashara ikiwa pamoja na kuwa balozi wa kitu fulani na hivyo hata kipato kikaongezeka".

Alisema kuwa pia ni fani ambayo inachangamoto nyingi na inatakiwa kwa wahusika kukabiliana nazo huku akiwasihi zaidi kuwa kikubwa wanachotakiwa kufanya ni kuwa na nidhamu na unyenyekevu. 

Vijana hao zaidi ya 15 wanafundishwa fani hiyo na kampuni ya Black Fox Models kila Jumapili katika mgahawa wa Paparazi uliopo Sleep way Masaki.

Mmilikiwa kampuni hiyo AJ Mynah alisema kuwa vijana wengi kwa sasa hapa nchini wamekuwa na hamasa ya kujihusisha na kazi mbalimbali zitokanazo na fani ya uanamitindo.

Alisema kuwa kikwazo kikubwa ni wengine kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na fani hiyo hasa kuanzia elimu yake kwa ujumla hadi namna ya kuifanya kazi yenyewe.

"Najua kumekuwa na mtazamo kuwa wanamitindo ni watu fulani wembamba, warefu na wazuri sana ila kumbe inawezekana hata ukawa wa kawaida ila ukawa na kitu fulani katika mwili wako ambacho unaweza kujivunia na kikatumika hata katika matangazo mfano mtu anakuwa na macho, au mdomo au hata kitu chochote ambazo anaweza kutumia kutangaza" alisema AJ.
===========

0 comments:

Post a Comment