Help Children
Love them
Saidia Watoto

Thursday, October 2, 2014

Penzi la nguruwe lamsitisha masomo

Picha ya Maktaba




UNAWEZA kudhani ni Hekaya za Kusadikika! Lakini ni  kisa  cha kweli kwamba, mama mzazi  amemshitaki polisi mwanaye wa kiume ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili mwenye umri wa miaka 16 kwa kile anachodai amechoshwa na tabia ya mwanaye ya kufanya mapenzi na  nguruwe  wao  jike  mara kwa mara na hata kujikuta akiacha shule.
 
Amelalamika akidai kuwa kijana huyo amenogewa `penzi’ la mnyama huyo maarufu hapa kama “kitimoto au Noah” kiasi cha kumfanya aache masomo na   kuwa mtoro sugu shuleni.

Nguruwe huyo  jike  inadaiwa  anafugwa  na  familia  ya mwanafunzi huyo anayesoma katika  shule moja  ya umma  ya sekondari, Manispaa  ya Sumbawanga.

Hayo yamethibitishwa na Mkuu wa Kitengo  cha Polisi Jamii  mkoani Rukwa, Sixmund Kibassa  aliyemweleza mwandishi  wa habari  hizi  jana kuwa, mama mzazi wa mtoto  ameripoti tukio hilo katika jeshi polisi. 

Kibassa amesifu uamuzi huo, akisema ni mafanikio  makubwa  yanayotokana na Mpango Shirikishi wa Kitengo  hicho  wa kurejesha  shuleni watoto  ambao ni watoro  sugu.

Anasema mwanafunzi  huyo  (jina limehifadhiwa) ni miongoni mwa watoro sugu 70 kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari katika Manispaa  ya Sumbawanga waliorejeshwa hivi karibuni kupitia mpango huo shirikishi wa kuwarejesha  watoro  shuleni  unaotekelezwa na Kitengo  cha Polisi Jamii  mkoani humo.

Kwa mujibu  wa Kibassa,  wazazi  na walezi wenyewe  wanafika katika kitengo  hicho  cha polisi  jamii  na kuripoto  kuhusu   watoto  wao  ambao  wamekatiza masomo .

Aliongeza kusema kuwa,  wazazi  na walezi hao  wanafichua ya kwamba watoto  wao hao  licha  ya kutokwenda shuleni, lakini pia nyumbani hawaonekani kwamba baadhi yao wamebainika kutumia muda wao  mwingi  kunywa pombe  vilabuni badala  ya kusoma.

“Sasa  hivi  karibuni  ni  juzi  tu  mama mmoja  alinifuata  na kuniripotia  kisa  cha mwanae wa kiume  anayesoma Kidato cha Pili  katika shule moja ya sekondari kwamba  licha ya kuwa mtoro sugu shuleni; lakini  pia  amekuwa na tabia   chafu  ya kufanya  mapenzi  na nguruwe  wao  jike   mara kwa mara …. Nilipomhoji kijana  huyo  alikiri kufanya hivyo …. basi  tulimnasihi, “ alieleza.

Kwa mujibu  wa Kibassa  baada ya kumsihi  mwanafunzi  huyo alikubali  kuendelea na masomo  ambapo  alirejeshwa shuleni kwake  na kupokelewa  na walimu  na wanafunzi wenzake  kwa furaha.

Daktari wa Tiba  ya Binadamu, Dk Paulo Maiga  akizungumzia tukio hilo alikiri  kuwa  mwanadamu  kufanya mapenzi  na mnyama kuna madhara makubwa ikiwemo  kuambukizwa  virusi  ambavyo  vikingia  mwilini mwa  binadamu  kuna uwezekano mkubwa  visiweze kutibiwa .

“Hili  ni tatizo  kubwa madhara  yake ni makubwa  huyu nguruwe anaweza kuwa  ameshambuliwa na  virusi vya ugonjwa  ambao ukiingia  na kumshambulia  mwanafunzi  huyo  upo uwezekanao  mkubwa  kusiwepo na tiba,“ alisisitiza Dk. Maiga.


0 comments:

Post a Comment