MSANII wa
muziki wa kizazi kipya Nicki wa Pili ameelezea nia yake ya kuandaa mradi maalum
wa kusaidia vijana katika masuala ya elimu.
Ni wa Pili
alisema kuwa anatarajia kuanzisha kitu kama vile kijiji cha elimu ambapo vijana
watakuwa wakikutana kujadili masuala ya elimu.
Alisema kuwa
pitia mradi huo vijana wataongeza hamasa ya kujisomea kwa kuwa watakuwa
wakikutana muda wote kujadili masuala ya elimu.
" Mradi
huu utafanyikia hapa Dar es salaam na ndio itakuwa ni njia rahisi ya kuwaongezea
hamasa sio tu wanafunzi bali hata wazazi wao ambao wengine hawajahamasika
katika masuala ya elimu"alisema Niki wa Pili.
Aliongeza
kuwa kufeli kwa wanafunzi kunatokana na kukosekana sio tu kwa msukumo kwenye
jamii lakini pia hata kukosekana kwa mkakati endelevu wa kuwasaidia vijana hao.
===========
0 comments:
Post a Comment