Na Mwandishi wetu
KAMPUNI ya simu ya Airtel inatarajia kuanza awamu ya mpya ya mpango wake wa kusaidia maendeleo ya elimu nchini kwa kusaidia upatikanaji wa vitendea kazi pamoja na kuboresha miundo mbinu ya shule za sekondari hapa nchini ujulikanao kama Airtel shule yetu.
Kwa kuanzia Airtel tayari imeshakarabati majengo ya shule ya msingi
Kiromo iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Meneja wa huduma za jamii wa Airtel Tanzania Hawa Bayuni alisema: “Airtel tunaingiakatika awamu mpya ya utoaji wa vitabu kwa shule zingine zaidi ya 150 zilizopo hapa Tanzania zilizopendekezwa na Wizara ya Elimu Tanzania kuwa ni shule zenye uhitaji zaidi na kushauri ziingie katika mpango wa kusaidia jamii wa Airtel shule yetu”
Tangu mradi wa vitabu uanze miaka nane iliyopita wameweza kuwafikia zaidi ya shule 1,500 za sekondari zilizopo Tanzania.
Aidha Airtel imekarabati miundombinu ya shule kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini kwa lengo kutimiza dhamira yetu ya kukuza kiwango cha elimu kwenye maeneo mbalimbali Tanzania aliongeza
Bayumi.
Mwaka jana shule tatu katika kila mkoa zilibahatika kupata msaada wa vitabu kutoka Airtel.
Mwaka huu vitabu watakavyogawa vinakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 120, hivyo kila shule itakayopatikana kupitia droo
tutakayochezesha mwezi huu wa tano wataweza kufaidika na mradi huu.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment