Mwenyekiti wa Havillah Africa Sports Academy (HASA) Davis Mkony (katikati)wakati akipokea msaada wa mifuko 50 ya saruji iliyotolewa na duka la Mummy's lilipo Mlimani City anaekabidhi ni mwakilishi kutoka duka hilo Sam Mphungu alisema Mwenyekiti wa Havillah Africa Sports Academy (HASA) Davis Mkony akiwa na wadau wengine wa Mradi huo wa Hasa.
Na Evance
Ng'ingo
WAFANYABIASHARA
na Makampuni mbalimbali yameombwa kuwekeza fedha zao kwenye michezo wa kusaidia
ujenzi wa vituo mbalimbali vya michezo nchini.
Hoja hiyo
ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Havillah
Africa Sports Academy (HASA) Davis Mkony wakati akipokea msaada wa mifuko 50 ya
saruji iliyotolewa na duka la Mummy's lilipo Mlimani City .
Msaada huo
ni kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha michezo maalum kwa ajili ya watoto waishio
mazingira magumu kwa lengo la kukuza vipaji vyao.
Mkony
alisema kuwa makampuni makubwa yanatakiwa kutambua kuwa kwa kuwekeza michezo
kwa watoto wadogo hususan wa mitaani itasaidia kuimarisha mazingira mazuri ya
biashara zao.
Alisema kuwa
michezo ndio njia pekee ya kuwanusuru watoto hao kujiingiza katika majanga
mbalimbali pindi wawapo wakubwa.
Akizungumzia
maandalizi ya mradi huo wa michezo kwa
watoto unaojengwa katika eneo la Mkuza
Mkuranga, Mkonyi alisema kuwa mradi huo unatarajia kukamilika Novemba mwezi
huu.
Alisema kuwa
unahusisha ujenzi wa majengo makubwa mabweni ya kulala watoto hao pamoja na
madarasa.
Alisema kuwa
tayari wameshanunua hekari 400 ambazo zinamilikiwa na mradi huo na kwa sasa
wameanza mchakato wa kulitayarisha vema eneo hilo.
" Najua
michezo ni kiwanda ambacho kinaweza kuzalisha mamilioni ya fedha kutoka kwa
watoto na nchi inaweza kutambulika kimataifa zaidi kupitia michezo
hiyohiyo" alisema Mkony.
Alifafanua
kuwa mradi huo unalenga pia kusambaa nchi nzima kwa lengo la kutafuta na
kuendeleza vipaji vya watoto hao na kuongeza kuwa ndani ya miaka ijayo watoto
hao wanaweza kufika katika anga la kimataifa zaidi.
Naye
mwakilishi kutoka duka hilo Sam Mphungu alisema kuwa likiwa kama duka kubwa la
mavazi linatambua umuhimu wa michezo katika kusaidia kukua kwa jamii.
"
Tulipopata maombi kutoka kwa hawa watu wa HASA kutuomba tusaidie harakati zao
hizi za kukuza vipaji vya watoto tulichukua uamuzi wa kuwasaidia kwa moyo mmoja
na tutaendelea kufanya hivyo" alisema Mpunghu.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment