Help Children
Love them
Saidia Watoto

Tuesday, April 16, 2013

Wanafunzi wa Veta changamkieni dili hili



WAHITIMU wa Mamlaka ya Ufundi Stadi nchini (VETA) watanufaika na makubaliano kati ya Shirikika la Nyumba la Taifa (NHC) na VETA kufuatia makubaliano waliyosaini ya kutoa mafunzo kwa vijana ya kutumia mashine za kufyatua tofali ambazo zitasadia shirika hilo kujenga nyumba za gharama nafuu.

 Akizungumza jana Mkurugenzi wa NHC, Nehemia Mchechu alisema kipaumbele cha shirika lake ni kujenga nyumba za gharama nafuu na njia ya kuhakikisha wanapunguza gharama za ujenzi ni kutumia matofali yanayotumia saruji kidogo na udogo lakini zenye ubora.

“Ukiangalia nyumba za kipato cha chini za Kibada (Dar es Salaam) ziliuzawa kwa sh milioni 39 bila kodi na hili limelalamikiwa sana, lakini mikakati yetu ya kujenga nyumba gharama nafuu imekutwa na changamoto ya upatikanaji usioridhisha wa vifaa nafuu vya ujenzi.

Mchechu aliongeza: “Katika kuondoa changamoto hii kwa kuanzia NHC imenunua mashine 15 za teknolojia ya Hydraform ili kurahisisha na kuharakisha upatikanaji wa matofali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu.

Mashine ya Hydraform zinauwezo wa kufyatua tofali 2000 kwa siku, hupunguza gharama za ujenzi kwa kutumia saruji wakati wa kutengeneza matofali, na hutumia lita 10 za mafuta kwa siku na urahisi wa kuzibeba mashine hizo na kutumia malighafi zinazopatikana eneo husika.

Mchechu alisema mbali na makubaliano hayo kuongeza ajira kwa vijana, lakini itasaidia upanuzi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu hivyo kuwawezesha wananchi wengi zaidi kumudu miliki ya nyumba hivyo kupunguza uhaba wa nyumba uliopo ambao kwa hivi sasa unafikia uhaba wa nyumba milioni 3.

“Manufaa yake ni makubwa kwani unatarajia kuwezesha ujenzi wa nyumba 1054 ndani ya mwaka mmoja ambapo jumla ya matofali 5,270,000 yenye gharama ya sh bilioni 3.162 yatatengenezwa katika mpango huo.”

Naye Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Zebadiah Moshi alisema mpango huo utasaidia mamlaka yake kuongeza ajira kwa vijana waliopata mafunzo katika vyuo vyao kutoka asilimia 66 ya sasa hadi asilimia 95 baada ya miaka mitano ijayo.

Moshi aliwaasa vijana hao kwa kusema: “mmepeta nafasi hii hakikisheni mnakuwa waadilifu na bidii ya kazi kwani baadhi yenu mnakosa kazi kutokana na kutokuwa waadilifu.”

Mkurugenzi wa Ujenzi NHC, Benedict Kilimba alisema wanafunzi hao 35 wamechanguliwa kutoka kwenye vyuo mbalimbali vya Vita na watapewa mafunzo hayo kwa wiki mbili kabla ya kupelekwa kwenye miradi ya ujenzi wa nyumba ya NHC inayofanyika kwenye mikoa 14.

0 comments:

Post a Comment