WANAFUNZI wa vyuo mbalimbali
nchini wametakiwa kuhakikisha wanafuata maadili, taratibu na sheria
wakati wanapoenda kufanya kazi kwa vitendo (Field) katika taasisi mbalimbali.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa
viwango vya Elimu na Ustawi wa Jamii Tanzania (TESWEP) Dk. Naftal Ng’ondi,
ambaye pia ni Mhadhiri wa chuo cha ustawi wa jamii, katika warsha ya wahadhiri.
“Wahadhiri nyinyi ndiyo mnatakiwa kuwa
mstari wa mbele kuwaelimisha wanafunzi wenu huko vyuoni kuhusu sheria na
maadili kwani kutokana na kukua kwa Teknohama, wanavyuo wamekua wakishindwa
kufuata miiko katika jamii,” alisema Ng’ondi.
Alisema katika utafiti wa TESWEP
umegundua kuwa katika makampuni mbalimbali wanavyuo wengi wanaokwenda kujifunza
kwa vitendo wamekuwa wakikiuka taratibu zilizowekwa na taasisi husika na mwisho
wa siku chuo husika kinalaumiwa kwa kutofundisha maadili kwa wanafunzi.
"Hawaheshimu waajiriwa wala
muda wa kufika kazini hauzingatiwi jamani hali hii inatoa taswira mbaya sana
katika vyuo vyetu hivyo inabidi tuwaelimishe vya kutosha, unakuta mvulana
anashusha suruali 'mlegezo' na mwanamke naye anavaa sketi fupi 'kimini'
wabadilisheni|” alisema mwenyekiti huyo.
Kwa upande wake Mratibu wa
mafunzo hayo Furaha Dimitrios, amesema jamii yoyote isiyokuwa na maadili ina hatari
kubwa hasa katika kipindi hiki cha ulimwengu huu wa sayansi na Teknologia.
"Sisi sote tunajua kuwa
maendeleo ya jamii kwa sasa ni makubwa hivyo yatupaswa kukabiliana nayo kwa
kuwa utandawazi ni mpana zaidi na wanafunzi wanatambua mambo mengi zaidi,”
alisema Dimitrios
Pia aliwataka wanafunzi wanapoenda
kufanya mafunzo kwa vitendo wajue kuwa ni maandalizi ya kazi wanayotarajia
kwenda kufanya hivyo ni jukumu lao kuvumilia na kukabiliana na changamoto
wanazokutana nazo.
mwisho
0 comments:
Post a Comment