WANAFUNZI 1,605 sawa na
asilimia 35 ya waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka huu katika
Wilaya ya Urambo, mkoani Tabora, wameshindwa kuripoti shuleni.
Ofisa Elimu Sekondari, wilayani
Urambo, Grace
Monge, alisema idadi hiyo ambayo hawajajiunga na masomo, ni sehemu
ya wanafunzi 4,604 waliochaguliwa kujiunga na sekondari mwaka huu.
Alifafanua kwamba kati ya hao ambao hawajajiunga, wavulana ni 805
na waliobaki ni wasichana.
Kwa mujibu wa Ofisa Elimu, miongoni mwa sababu za wanafunzi
kutoripoti ni baadhi yao kuolewa mapema,
kukosa ada na mahitaji muhimu yanayotakiwa shuleni kutokana na
umasikini wa wazazi.
Sababu nyingine ni wazazi kuwatumikisha watoto wao katika
shughuli za kilimo hasa tumbaku na wengine kuwazuia ili waongeze
nguvukazi katika kilimo.
0 comments:
Post a Comment