WABUNGE wanaotoka mikoa ya Kusini ya Lindi na Mtwara wametakiwa
kutetea haki za watoto ikiwemo kuishauri Serikali kurudisha shule za wasichana
za Mtwara na Masasi zitoe elimu kuanzia
kidato cha kwanza hadi cha nne badala ya kidato cha tano na sita.
Hayo yalisemwa juzi na
mmoja wa washiriki kutoka Kanda ya Kusini, Bibiana
Mmoro wakati wa kongamano la Kitaifa la Wanawake, lililoandaliwa
na Muungano wa Mashirika ya kutetea masuala ya jinsia lililomalizika jana mjini
Dodoma.
Mmoro alisema kuwa, shule hizo mbili zilikuwa zikisaidia kwa
kiasi kikubwa kupokea watoto wa Kusini lakini baada
ya kubadilishwa kuwa
kidato cha tano na sita wengi wanaochaguliwa wanatoka nje ya Kanda
ya
Kusini.
Pia, alitaka wabunge kutetea haki za watoto kwa kuhakikisha kila
wilaya
inakuwa na shule moja ya bweni ili kuwapa fursa wanafunzi wengi wa
kike
kupata elimu bora.
Mbunge wa Viti Maalumu Agnes Hokororo (CCM) alisema masuala ya
siasa
yamekuwa yakirudisha nyuma maendeleo kwa wananchi kupiga vita
baadhi ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.
0 comments:
Post a Comment