IMEELEZWA kutokana na asilimia kubwa ya
wazazi kutojua kusoma na kuandika, wamekuwa wakishindwa kuchangia michango
mbalimbali ya maendeleo ya elimu ili kukuza sekta hiyo ambayo imeonekana
kushuka.
Hayo yameelezwa na mkuu wa wilaya ya
Mkuranga, Mercy Silla wakati wa ufunguzi wa bweni la wasichana katika sekondari
ya Vianzi iliyopo tarafa ya Vianzi wilaya ya Mkuranga ambapo limegharimu Sh 88 milioni
hadi kukamilika kwake.
Silla alisema asilimia 57 ya watu wazima
katika wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani hawajui kusoma na kuandika hali
inayopelekea wazazi hao washindwe kuchangia maendeleo ya elimu kutokana na
kutojua nini umuhimu wa elimu.
Alisema wazazi wanatakiwa kujenga
utamamduni wa kuchangia maendeleo na sio kusubiri wahisani na wafadhili
mbalimbali kuja kutoa misaada ya maendeleo ya elimu.
“ Huu ni wakati kwa wazazi
kujenga utamaduni wa kuchangia miradi ya maendeleo ya elimu na sio kusubiri
misaada toka wahisani na wafadhili”alisema.
Naye Mkurungezi Mkuu wa Mamlaka ya
Elimu nchini(Tea) Rosemary Lulabuka alisema lengo la kujenga bweni hilo ni
kusaidia watoto wa kike ambao wanapata shida ya kutembea umbali mrefu kutoka
nyumbani hadi shuleni hapo.
Lulabuka alisema bweni hilo
lilikamilika mwishoni mwa mwaka juzi lakini halikuweza kutumika kutokana
na uwezo mdogo wa wananchi katika kuchangia ununuzi wa vitanda na magodoro.
“Bweni lina jumla ya vitanda 36
vya juu na chini(Double decker) vyenye magodoro 72 na linachukua
wanafunzi 72 na lina mabafu matano na vyoo nyeye matundu matano, pia mamlaka
yangu imejitolea kufunga umeme wa jua kwa ajili ya wanafunzi hao kujisomea
wakati wa usiku” Alisema Lulabuka.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment