Wadau wengi wa elimu walijitokeza |
Wahadhiri pia walikuwapo |
Watoa mada |
Mbati hakukosekana |
Habari kutoka gazeti la HabariLeo
MDAHALO wa kitaifa wa elimu uliofanyika jana
umebainisha kiini cha kuporomoka kwa kiwango cha elimu nchini ambacho ni
walimu, viongozi wa serikali, wananchi na wazazi kwa ujumla.
Akichokoza mada kwenye mdahalo uliofanyika kwenye
Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitila Mkumbo alisema utafiti
walioufanya unaonyesha kuwa shule zinazofundishwa walimu wenye sifa ndizo
ambazo hazifanyi vizuri kuliko zile zinazofundishwa na walimu wenye stashahada
na wanaofundisha kwa kuwa na leseni pekee.
Alisema kuwa katika utafiti huo waliuliza maswali
mawili ya kwanini wamechangua kusomea fani ya uwalimu na je wanampaka wa kukaa
kwa muda gani kwenye taaruma na majibu hayo yaonyesha wale wenye elimu ya
stashahada walikuwa na uhakika wa kuendelea kufundisha kuliko wale wenye
shahada.
“Shule ya
Mukoba (mwenyekiti wa CWT-Gracian) ni miongoni mwa shule zenye walimu wengi
wenye sifa, lakini inawanafunzi wengi wenye divisheni 0, lakini shule kama
Maria inawanafunzi wenye stashahada wanafany vizuri.
Mkumbo aliongeza: “Ningekuwa ni Waziri wa Elimu
ningeajiri walimu wenye diploma (stashahada) na kuachana na wenye shahada maana
hawa hawatulii na wengi wao walipojiwa walisema kama ukimaliza kutohoji
ikatokea kazi naondoka sasa hivyi.”
Mkumbo alisema pia udogo wa mishahara kwenye shule
za umma ndizo zinazowafanya walimu wengi kutotulia shuleni kuliko wale
wanaofundisha katika shule za watu binafsi na mashirika ya dini.
“Katika wagonjwa elimu wa Afrika, sisi tunakaribia
kutoka wodini kwasababu tumefanikiwa katika kuingiza watoto wengi shule ya
msingi, sekondari na katika vyuoni.
Ni lazima tuwekeze sana kwenye elimu kwasababu
ni taifa la watoto kwani asilimia kubwa ya vijana. Hata tukijivunia kuwa tuna
gesi tukiwa hatuna akili gesi itatulipukia,” alisema.
Aidha alisema kunahatari kubwa ya mwaka 2015 kwa
vyuo binafsi kukosa wanafunzi kufuatia matokoe ya kidato cha nne ya mwaka jana
na kushauri kuwa wale waliopata daraja la tatu bila kuwa na alama nzuri wapewe
mafunzo maalumu na wale wa kidato cha nne wafundishwe na kurudia mtihani na
wale waliopata daraja sifuri warudie kwa nguvu zao wenyewe.
Naye mtaalamu wa mipango ya elimu na utawala,
kubuni program na tathimini profesa Herme Mosha alisema mfumo wa kuwachagua
wanafunzi wanaokwenda kusomewa uwalimu wakiwa ni wale wasiofanya vizuri kwenye
mitihani yao kwani watu hao wanakuwa na upungufu wa maarifa kwa asilimia 70
hivyo vigumu katika kuwafanya watoe wanafunzi wenye alama A.
Mkumbo alisema kunahaja ya kuweka suala la elimu
kuwa kipaumbele cha taifa na na kuwekeza katika elimu huku akinukuu viongozi
mbalimbali akiwamo Hayati Mwalimu Julius Nyerere, na Waziri Mkuu wa Uongereza
Tony Blaia waliozungumza na kutilia mkazo suala la elimu huku Rais Benjamini
Mkapa kipaumbele chake kuwa ni uchumi.
Akimnukuu nyerere “ atuna jaha ya kutozungumzia
elimu na mataifa makubwa yataumia elimu kama nyenzo kuu ya kutugandamiza.”
Akinukuu Blair alisema “ukiniuliza tena kipaumbele
katika sera yangu ni elimu, elimu elimu wakati Rais mstaafu Benjamini Mkapa
alisema kipaumbele change ni uchumi, uchumi, uchumi.
Akitoa mada ya usawa, fulsa na ubora wa elimu
Profesa Adolf Mkenda alisema viongozi wengi hawaweki kipaumbele katika elimu
“ Wanaopigia kelele sera na kuzisimamia watoto wao
hawasomi kwenye shule hizo, wenzetu Uingereza Tony Blair walimuhoji ni kwanini
watoto wake hawasomi shule za umma lakini je hapa tunaweza kuhoji?
Mkenda alioongeza: “Mtu anayesimamia kitu ambayo
hakimuusu moja kwa moja je anaweza kuwa na nafasi ya kufanya vizuri?”
Hata hivyo, kuwa kuna haja ya walimu kuongezewa
mishahara kuliko ilivyo sasa kwani hali hiyo inachangia kuzorotesha mori wa
kufundisha.
Akitolea mfano, Mkumbo alisema walimu waliomaliza
shahada ya uwalimu kwa miaka mitatu huwanza na mshahara mdogo ukilinganisha na
taaluma zingine na pia kushauri kuwapo
kwa shule maalumu za kitaifa ambazo zitasimamiwa na wizara na kuwa shule za
kata zibaki mikononi mwa halimashauri
Haidham watu mbalimbali waliochangia madahalo huo
wametaka kuwapo ushirikiano kati ya walimu na wazazi katika suala zima la elimu
kwa mwanafunzi na kuonya kuacha kuwa buzy kutafuta ada bila kujua elimu
wanayopata watoto zao.
0 comments:
Post a Comment