Help Children
Love them
Saidia Watoto

Friday, April 26, 2013

Nipo mikoani katika ziara za kikazi kuhusiana na masuala ya elimu

Nakaribishwa katika maktaba moja ipo Saadani vijijini mkoani Tanga

Hapa ndipo anapoweka vitabu vyake huyu mmiliki wa maktaba hiyo

Hap ndipo kwa ndani ya maktaba yake ambapo anafundisha na kuwapatia wanafunzi fursa ya kusoma vitabu bure

                                       Hili ni darasa lililopo Saadani katika mbuga kabisa
Wanafunzi wakichota maji

Wednesday, April 24, 2013

Mwanafunzi Arusha auwawa na wezi, wenzao waanzisha vurugu kubwa inaendelea hadi sasa

Henry aliyeuwawa

Lema akiwatuliza wanafunzi waliolianzisha baada ya mwenzao kufa
Mbunge Wa Arusha Mjini Godbless Lema Akiwatuliza Wanafunzi Wa Chuo Hicho
----

Taarifa Kutoka  Chuo Cha Uhasibu Arusha zinadai kuwa Mwanafunzi Wa BEF 2  anayejulikana  kwa  jina  la  Henry  ameuawa  kikatili  na  watu  wasiofahamika....

Mwanafunzi  huyo  Alikuwa Masomoni Mida Ya Usiku Na Alipomaliza Aliondoka Na Kuelekea Maeneo Ya Esami. Kabla Hajafika Eneo La Malazi (Hostel) alipigiwa Simu na Mwenzake amsubiri Ili Waende Wote Hostel.  
 
 Inasemekana Wakati anamsubiri Rafiki Yake Kwenda Hostel, Kuna Bajaj Ilifika Eneo Hilo Na Watu Hao Wasiojulikana Wakataka Pesa Kutoka Kwa Mwanafunzi Huyo...Wakati  wakiendelea  kuzozana, rafiki  yake  naye  alifika.....
 
Majibu Ya Wanafunzi Hao Hayakuwafurahisha Watu Hao Na Ndio Walipochomoa Kisu Na Kumchoma Mmoja wa Vijana Hao Tumboni Na Shingoni na Kupoteza Maisha Hapo Hapo....

 
Rafiki Aliye Kuwa Nae Inasemekana Alichomwa Kisu Cha Tumboni Na Kuachwa Akishuhudia Mwenzake Akipoteza Maish

Sunday, April 21, 2013

Habari ya elimu kama ilivyojitokeza katika Habari Leo ya Leo

Serikali yarudi katika
mazungumzo na walimu
*Yaahidi mishahara bora watumishi wa chini
*Yahoji kuhusu nia njema ya Mukoba wa CWT
*Ni kwa kupotosha ukweli wa mazungumzo
Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imerejea katika meza ya mazungumzo na Chama cha Walimu Tanzania (CWT), pamoja na kutokuwepo kwa mazingira ya nia njema kutoka upande wawawakilishi wa walimu katika mazungumzo hayo.

Taarifa ya Ikulu iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, ilieleza kwamba Serikali imefikia hatua hiyo, ili kuonesha utayari na nia njema katika mazungumzo hayo.

Mbali na utayari, pia Serikali imetangaza kwamba kutakuwepo na nyongeza nzuri kwenye mishahara, hasa ya watumishi wa ngazi za chini katika mwaka ujao wa fedha. 
Kabla ya hatu hiyo, vyombo vya habari vilimkariri Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba
akisema kwamba Serikali imekataa kukaa meza moja na CWT, ili kuzungumzia nyongeza ya mishahara na posho za walimu, pamoja na kwamba chama hicho chenyewe kiko tayari kwa mazungumzo.

Mukoba pia alikaririwa akidai kwamba Serikali imepuuza amri ya Mahakama, inayotaka pande hizo mbili kukaa meza moja kujadili madai ya walimu.

Kutokana na madai hayo, Mukoba alilitaka Bunge na wazazi, kuingilia kati uamuzi wa Serikali kukataa kukaa meza moja na CWT.

Nia njema
“Serikali inapenda kuwafahamisha wananchi kuwa, madai haya yote hayana chembe ya ukweli, na hayana nia njema, maana yanaweza kujenga chuki na mazingira ya kuzua mgogoro mwingine na Serikali usio na sababu, wala maslahi kwa walimu wenyewe na Taifa,” imeeleza taarifa hiyo ya Ikulu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Serikali imeeleza kuwa haijakataa majadiliano na CWT, na wala haijapuuza amri ya Mahakama inayotaka pande zote mbili kurudi kwenye meza ya majadiliano. 

Tofauti na madai ya Mukoba, taarifa ya Serikali ilieleza kuwa tangu amri ya Mahakama itolewe, tayari vimefanyika vikao vinne vya Baraza la Majadiliano ya Pamoja katika utumishi wa walimu. 

“Vikao viwili vilifanyika mwaka jana Septemba 12, na  Desemba 5. Vikao viwili tayari vimefanyika mwaka huu Januari 9-10 na Machi 22,” ilieleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilifafanua kwamba kilichochelewesha suala la mishahara na posho kujadiliwa katika vikao hivyo, si kwamba Serikali haikutaka mjadala huo. 

“Sababu hasa ni kuwa CWT ilikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu, katika kesi Na. 96/2012, na Serikali iliwasihi viongozi wa CWT wafute rufaa hiyo, ili kuruhusu majadiliano ya mishahara na posho, lakini walikataa. 

“Kitendo hicho hakioneshi nia njema upande wao. Nia njema ni sharti muhimu kwenye majadiliano haya. Kwa upande wake, ili kuonesha utayari na nia njema, Serikali sasa imekubali majadiliano hayo yaendelee, licha ya CWT kukataa kufuta rufaa yao,” ilieleza taarifa hiyo. 

Serikali imeelezea sababu ya pili iliyochelewesha majadiliano ya maslahi ya walimu, kuwa ni madai ambayo awali viongozi wa CWT walikuja nayo kuwa iteuliwe timu maalum ya kuzungumzia maslahi, badala ya Baraza la Majadiliano ya Pamoja katika utumishi wa walimu, ambalo ndilo lipo kisheria kwa majadiliano hayo. 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, CWT ilichelewa kurejesha majadiliano kwenye Baraza hilo, mpaka wakati wa kikao cha Januari 9 hadi 10, mwaka huu.

Uzushi wa Mukoba
Wakati Mukoba alikaririwa kwamba kikao kilichokataa kuzungumzia mishahara na posho za walimu, ni  kilichofanyika Aprili 2 mwaka huu, chini ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, Serikali imepinga madai hayo.  

“Si kweli vilevile kuwa kikao kilichofanyika Ikulu, Aprili 2, mwaka huu chini ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi  Sefue, ndicho kilikataa majadiliano kuhusu maslahi ya walimu. 

“Kauli hiyo ni upotoshaji wa makusudi usio na nia njema. Viongozi wa CWT wanajua vema kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, si sehemu ya mfumo wa majadiliano kuhusu maslahi ya walimu. Hivyo, kikao kinachoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi, hakiwezi kuwa mahali pa majadiliano ya mishahara, posho na maslahi ya walimu,” ilieleza taarifa hiyo. 

Ilifafanuliwa kwamba mkutano huo wa Aprili 2, uliitishwa na Katibu Mkuu Kiongozi kwa maombi rasmi yauongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), ambao walitaka kujulishwa jinsi utaratibu wa majadiliano ya mishahara ya wafanyakazi wote utakavyokuwa, kutokana na kuanzishwa kwa mzunguko mpya wa Bajeti ya Serikali.
Serikali imeeleza kuwa kikao hicho kisingeweza kugeuka na kuwa kikao cha kujadili mishahara na posho za walimu, kama alivyokaririwa Mukoba akidai.

“Tunapenda wananchi na walimu wajue pia kuwa Gratian Mukoba, hakuwepo kwenye hicho kikao cha Aprili 2, 2013. Aidha, kikao hicho kilikuwa cha Tucta, hakikuwa cha CWT,” ilideleza taarifa hiyo.

*Dhamira ya CWT
Serikali imeelezea kupata tabu ya kuelewa nia na dhamira ya viongozi wa CWT, kwa kupotosha kwa makusudi wananchi na walimu kwa mambo yaliyo wazi “Serikali imeonesha nia na dhamira ya wazi ya kujadiliana na CWT, pamoja na vyama vyote vya wafanyakazi, kuhusu maslahi ya wafanyakazi. 

Vikao vingi vilivyofanyika na vinavyoendelea kufanyika kwenye mabaraza ya kisekta na Baraza Kuu, ni ishara ya wazi ya nia njema ya Serikali. 

“Tunajiuliza, katika hali hiyo, juhudi hizi za viongozi wa CWT kuandaa mazingira ya mgogoro wa Serikali lengo lake ni nini hasa?” Ilihoji taarifa hiyo.

Saturday, April 20, 2013

Mwanafunzi aliyepua watu huko Boston Marekani aliyekuwa hajakamatwa sasa kashakamatwa

                                                        Huyu ndo alikuwa amebakia

HATIMAYE MTUHUMIWA WA PILI WA MIRIPUKO YA BOSTON ATIWA MBARONI


Mshukiwa wa mwisho katika utegaji wa mabomu yaliyowauwa watu 3 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 180 katika mbio za Marathon za Boston amekamatwa akiwa ndani ya boti. Polisi imesema kuwa amepelekwa hospitali akiwa mahututi.

Kukamatwa kwa mtu huyo Dzhokhar Tsarnaev, mwenye umri wa miaka 19 kumehitimisha operesheni kubwa ya siku nne, na kumekuja siku moja baada ya shirika la upelelezi la Marekani FBI kuchapisha picha za washukiwa hao.

Mshukiwa mwingine, Tamerlan Tsarnaev mwenye umri wa miaka 26 na ambaye ni kaka wa Dzhokhar, aliuawa jana Ijumaa katika majibizano ya risasi na polisi.

Kaka waripuaji: Tamerlan Tsarnaev (Kushoto) na mdogo wake Dzhokhar
Tamerlan Tsarnaev (Kushoto) na mdogo wake Dzhokhar

Umati wa watu katika mji wa Boston ulishangilia kwa shangwe baada ya kuibuka kwa ripoti ya kukamatwa kwa mshukiwa huyo. Shughuli zote katika mji huo zilikuwa zimesimamishwa wakati operesheni ya kuwasaka vijana hao ilipokuwa ikiendelea.

Bado yapo maswali yasio na majibu
Akizungumza muda mfupi baada ya kukamatwa kwa Dzhokhar Tsarnaev, rais wa Marekani Barack Obama alisema kukamatwa kwa mshukiwa huyo ilikuwa hatua muhimu katika mkasa unaohusu miripuko ya Boston.

Hata hivyo, Obama alisema kuwa bado yanabakia maswali yasio na majibu, ambayo ni pamoja na sababu iliyowafanya vijana hao kufanya mashambulizi, na ikiwa walikuwa na msaada katika uhalifu wao.

''Tutatathmini kilichotokea, na tutachunguza kama magaidi hawa walikuwa na washirika, na tutafanya chochote kinachohitajika kuhakikisha usalama wa watu'', alisema rais Obama.

Mripuko kwenye mbio za Marathon za Boston iliuwa watu 3 na kujeruhi zaidi ya 180

Polisi mjini Boston wamesema kuwa watu wengine watatu wamekamatwa na wanahojiwa kwenye nyumba aliyoishi Dzhokhar Tsarnaev karibu na chuo kikuu cha Massachusetts.

This image obtained April 19, 2013 courtesy CBS News shows Dzhokhar Tsarnaev, a suspect in the Boston Marathon bombing who was captured Friday night, April 19, 2013 after he was found hiding in a boat in a Boston suburb
Polisi wamesema walikuwa wakianza kukata tamaa katika operesheni yao, hadi pale walipopigiwa simu na raia ambaye ameiona damu kwenye boti yake, na kumkuta mshukiwa ndani ya boti hiyo akiwa ametokwa na damu nyingi.

Hisia kali dhidi ya Marekani
Watuhumiwa hao wametambuliwa kuwa ni jamii ya Chechen kutoka kusini mwa Urusi, ambao inaaminiwa wamekuwa wakiishi Marekani kwa muda wa miaka 10. Jimbo la Chechnya limeshuhudia vita viwili vikubwa tangu mwaka 1994, baina ya Urusi na wapiganaji wanaotaka kujitenga kwa jimbo hilo.

Kaka mkubwa Tamerlan anasemakana alikuwa na maoni makali dhidi ya Marekani, akiishutumu nchi hiyo kutumia Biblia kama kisingizio kuzivamia nchi nyingine.

Kabla ya kukamatwa kwa mdogo wake mji wa Boston ulikuwa umepooza, baada ya utawala kufunga barabara zote na kuwashauri wenye biashara kuzifunga. Hali kadhalika wakazi milioni moja wa mji huo na vitongoji vyake walikuwa wameombwa kubakia ndani ya nyumba zao, na kufungua mlango tu kwa maafisa wa polisi waliovali

Friday, April 19, 2013

Wanafunzi wanaodhaminiwa kusoma nje na kisha kufanya ugaidi wanawaalibia wengine

      Huyu ndo nuksi mwenye ambae alidhaminiwa kusoma Marekani na Kaka yake lakini ndo hao wamelianzisha
                                                                  Msako unaendelea
                                    Mpaka apatikane kwanza ni huyo dogo juu ndo bado yupo bro wake kashauwawa
                                                                  Vifaa vya  nguvu
                                                                  Full ulinzi

In May of 2011, Dzhokhar A. Tsarnaev, then a senior at a prestigious high school, was awarded a $2,500 scholarship from the city of Cambridge, Mass., to pursue higher education. Now, Tsarnaev is on the run, described as "armed and dangerous" and suspected of the Boston Marathon bombing.

Two brothers, one now dead, one alive and at large. After hours of only grainy images of two men in baseball caps to go on, a portrait gradually started emerging Friday of the men suspected in the attack.

Tsarnaev, 19, and his older brother, Tamerlan, who was killed during a violent night in Cambridge, had been living together on Norfolk Street in Cambridge. An uncle, Ruslan Tsarni of Montgomery Village, Md., told The Associated Press that the men lived together near Boston and have been in the United States for about a decade. They came from the Russian region near Chechnya, which has been plagued by an Islamic insurgency stemming from separatist wars.

Dzhokhar Tsarnaev's page on the Russian social networking site Vkontakte says he attended Cambridge Rindge and Latin School, graduating in 2011, the year he won the scholarship, which was celebrated with a reception at City Hall, according to a news release issued at the time.

 Before moving to the United States, he attended School No. 1 in Makhachkala, the capital of Dagestan, a predominantly Muslim republic in Russia's North Caucasus that has become an epicenter of the Islamic insurgency that spilled over from Chechnya. On the site, he describes himself as speaking Chechen as well as English and Russian. His world view is described as "Islam" and he says his personal goal is "career and money."

Tsarnaev appeared in the video released by authorities on Thursday, identified as Suspect Number 2, striding down a sidewalk, unnoticed by spectators who were absorbed in the race. He followed Tamerlan by about 10 feet. He wore what appeared to be a gray hoodie under a dark jacket and pants, and a white baseball cap facing backward and pulled down haphazardly.

Tamerlan was stockier, in khaki pants, a light T-shirt, and a dark jacket. The brim of his baseball cap faced forward, and he may have been wearing sunglasses.

According to the website spotcrime.com, Tamerlan was arrested for domestic violence in July 2009, after assaulting his girlfriend.

He was an amateur boxer, listed as a competitor in a National Golden Gloves competition in 2009.
_____

Tuesday, April 16, 2013

Wanafunzi yatima wapewa misaada


WANAFUNZI yatima na waishio kwenye mazingira magumu 80 wilayani Kyela wamepewa msaada wa sare na vifaa mbalimbali vya shule vikiwa na thamani ya jumla ya sh milioni nne.

Shirika la The Struggle for Community Support Alliance(SCSA) lenye makao makuu yake wilayani hapa ndilo lililotoa msaada huo uliokabidhiwa juzi ikiwa ni siku rasmi ya kuzinduliwa kwa mpango mkakati wa miaka mitano wa shirika hilo.

Vifaa vingine vilivyotolewa kwa wanafunzi hao ambao ni wa shule za msingi ni pamoja na daftari na kalamu za wino na risasi huku pia shule ya awali ya Itunge Education Point ya wilayani hapa pia akipewa msaada wa vitabu 20,mbao mbili za kuandikia na makasha ya chaki.

Kwa mujibu wa uongozi wa SCSA, wanafunzi waliopata msaada huo ni kutoka katika kata kumi za wilayani hapa ambazo ni pamoja na Makwale,Ndobo,Ipinda,Kyela mjini,na Ikana.

Kata nyingine ni Ipande,Ngana,Ikimba,Itope na Katumba huku kata nyingine zinazosalia zikitarajiwa kunufaika na msaada kama huo katika awamu nyingine zijazo.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Abraham Mwanyamaki alisema msaada huo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa shirika wa mwaka 2013/2017 ambapo zaidi ya bilioni mbili zinataraajiwa kutumika.

Mwanyamaki alisema mpango mkakati huo umejikita katika progamu nne alizozitaja kuwa ni Huduma za elimu,Huduma za afya vijijini,uwezeshaji jamii kiuchumi pamoja na uhifadhi wa mazingira.

“Tunaamini kuwa maendeleo ya wanakyela yataletwa na sisi wenyewe. Ndiyo sababu tumejikita katika kutatua changamoto zilizopo kwenye utekelezaji wa maendeleo wilayani hapa.Tulikwishatoa msaada wa dawati 100 na sasa tunaendelea”

“Tunapenda kuona wanakyela wananufaika na fursa zilizopo kwenye maeneo yao.Lakini pia jamii itambue kuwa utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo umekuwa chanzo kikubwa cha uharibifu wa mazingira yetu.Tunataka mambo haya yaende sambamba na utunzaji mazingira” alisema.

Hata hivyo Mwanyamaki alisema utekelezaji wa mpango mkakati wa  SCSA kwa kipindi cha miaka mitano unakabiliwa na changamoto nyingi zinazohitaji ushiriki wa wadau mbalimbali kuzitafutia ufumbuzi.

Baadhi ya wanafunzi waliopokea msaada huo,  Lucia Alphonce na Marium Benson walishukuru shirika hilo kwa msaada wa vifaa vya shule wakisema itakuwa chachu ya wao kujituma katika masomo yao kwakuwa watajiona hawako tofauti na wenzao.
mwisho







Mwalimu akutwa kafa



MWALIMU wa Shule ya Atlas,Elizabeth Mbaga (22) mkazi wa Kimara Baruti amekutwa amekufa chumbani kwake na mwili wake ukiwa hauna jeraha lolote.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema mwili ulikutwa juzi saa 11:30 jioni. 

Ingawa Polisi imesema chanzo cha kifo hakijafahamika, taarifa kutoka kwa jamaa na majirani, kabla ya kubainika amekufa chumbani, jana yake usiku alitoka na rafiki yake wa kiume na haikufahamika walikokwenda. 

 “Juzi (Jumapili) usiku waliondoka hapa na mpenzi wake mwenye asili ya Kiasia. Lakini muda mfupi kabla ya kuondoka kulikuwa na kutoelewana,” alisema mmoja wa majirani ambaye hakutaka jina lake litajwe. 

Aliendelae kusema, “Hatukumuona mpaka walimu wenzake walipokuja jana hapa nyumbani na kukuta mwili wake kitandani huku mlango ukiwa umeegeshwa,” alisema mmoja wa majirani ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
  
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Shule ya Atlas, Zana Rugambwa, baada ya mwalimu huyo kutoonekana shuleni Jumatatu huku simu yake ikiwa haipatikana, walimu wenzake waliamua kumfuata nyumbani kwake na kukuta amefariki dunia. 

Mwili wa mwalimu huyo ambao umehifadhiwa hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi, unatarajiwa kuagwa leo katika shule ya Atlas Madale kabla ya kusafirishwa kwenda kwao Arusha.