Help Children
Love them
Saidia Watoto

Tuesday, July 2, 2013

Wasomi msikurupuke



WASOMI nchini wameaswa kufanya mambo kisomi na kuacha kufuata mkumbo kwa kushabikia mambo yanayotokea na kukurupuka kuzungumza bila kufanya utafiti wa kutosha.

Wito huo umetolewa jana na Mhadhiri wa Chuo kikuu Stella Maris cha Mtwara(STEMMUCO) ambacho ni Chuo Kikuu kishiriki cha St Agostine(Saut), Charles Buteta, alipokuwa anazungumza katika mahafali ya wahitimu wa chuo hicho ambao ni wanachama wa Chama cha Mapinduzi(CCM) tawi la chuoni hapo.


Buteta alisema katika siku za hivi karibuni kumezuka mtindo kwa wasomi kushabikia mambo na kutoa kauli kali ambazo zingepaswa kutolewa baada ya kufanyiwa utafiti wa kina jambo ambalo alidai linaweza kuyumbisha jamii na kuhatarisha amani ya taifa.

“Nawasihi ninyi msiwe kama wasomi wanaokurupuka na kuongelea mambo bila kuyafanyia utafiti maana watu wanatuamini sisi wasomi kuwa tunaona mbali
sasa inapotokea msomi unaongelea jambo ambalo hata hulifahamu au kwa sababu zako za kisiasa na kupotosha ukweli ni hatari,”alisema Buteta.

Mhadhiri huyo alisema ni vema wasomi wakawa wazalendo na kuitumia elimu yao waliyoipata kwa kodi za wananchi kwa manufaa ya wengi na si kuangalia maslahi yao ya kisiasa ili kuwasaidia kukabiliana na changamoto zinapojitokeza.

Naye Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara, Mohamed Sinani alisema chama chake kinajivunia wasomi walioko vyuoni hivi sasa na kinaamini watakuwa ni nyenzo muhimu katika kukisaidia chama hicho kuelimisha jamii juu ya masuala mabalimbali yanavyokwenda.

Sinani alisema iwapo wasomi hao watatumia elimu yao kuelimisha wengine kwa kutolea ufafanuzi wa mambo kwa kina na kitaalamu wanaweza kuwa msaada
mkubwa katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinapojitokeza.

“CCM ni chama cha watu wa kada zote lakini kwa kiasi kikubwa tunakutegemeeni ninyi wasomi kuyatolea ufafanuzi mambo yanayopotoshwa na watu wengine wasiokitakia mema chama chetu na serikali yake. Nendeni mkaishi kama wasomi mliokomazwa na ikitakadi njema ya amani na utulivu unafika kote duniani ambao unaimarishwa na CCM”, alisema.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi kukabidhi vyeti kwa wahitimu katika sherehe hizo, Mwenyekiti wa ccm tawi la STEMMUCO, Mariamu Abbas alisema wahitimu hao 114 ni kati ya wanachama 221 waliopo katika tawi hilo.


0 comments:

Post a Comment