11:03 PM
BARAZA la Elimu la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki (IUCEA) limesema mfumo wa elimu nchini umekuwa ukipoteza watu
wenye ujuzi wa mambo mbalimbali kwa
kigezo cha kushindwa katika mitihani ya kumaliza masomo.
Katibu
Mtendaji wa wa baraza hilo, Profesa Mayunga Nkunya alisema wanafunzi
wasihukumiwe kwa kushindwa mtihani bali aangaliwe upande mwingine, ni nini
anaweza kufanya kuinua uchumi.
“Utaratibu
wa sasa wa elimu unakotupeleka hakufai kabisa…kigezo cha kuangalia kufaulu ama
kufeli tu kwa mwanafunzi sio suala jema kwani wapo wengi wanaokuwa wavumbuzi na
wenye ujuzi mbalimbali ambao hawapewi nafasi,” alisema Profesa Nkunya na
kutaja, Rwanda kwamba wanaotekeleza
mfumo unaompandisha mtu alipo bila kuangalia mtihani.
Profesa Nkunya alisema hayo Dar es Salaam wakati
akizungumzia ushirikiano uliopo kati yao na Baraza la Biashara la Afrika
Mashariki (EABC) katika kupambana na
ukosefu wa ajira kwa vijana.
Mabaraza
hayo yameandaa mkutano wa Afrika Mashariki wenye kujadili mahitaji ya soko la
ajira kwa kuzingatia taaluma. Mkutano huo utafanyika Oktoba 24 na 26 jijini
Nairobi, Kenya.
Alisema
Baraza hilo litatayarisha mkakati wenye kujikita zaidi katika kuangalia ujuzi
kwenye taaluma kama ilivyo Rwanda ambao utahakikisha suala la elimu linaendana
na ajira katika nchi hizo.
0 comments:
Post a Comment