Help Children
Love them
Saidia Watoto

Wednesday, July 17, 2013

DC aifunga shule ya mchungaji mbabaishaji, Shinyanga

Hii sio picha halisi ya shule hiyo

 MKUU wa Wilaya ya Shinyanga,  Anna- Rose Nyamubi ameifunga shule ya awali ya  Green Ihampa inayomilikiwa na mchungaji Yohana Japheth Nzuguni iliyopo kata ya Ndala manispaa  ya Shinyanga kutokana na mazingira yake kutoridhisha kwa watoto kulala chini.

Mkuu huyo akiwa na viongozi wa idara mbalimbali za manispaa pamoja na viongozi wa kanisa la Anglikana  Dayosisi ya Shinyanga, alifika juzi katika bweni wanamolala wanafunzi hao na kujionea hali ya mazingira isiyoridhisha kwa watoto 35 ambao wamekusanywa kutoka maeneo mbalimbali. 

 Mbali na watoto hao kulala chini, pia  bweni hilo halina huduma ya umeme, hali inayowafanya  kulala gizani huku wakiumwa na mbu kwani hakuna vyandarua na hata  madirisha ya bweni hilo hayajakamilika. 

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo hilo, Mkuu wa wilaya alisema hatua  ya kufunga shule hiyo ya awali inakuja kutokana na taarifa alizopewa na viongozi wa serikali ya mtaa huo wakishirikiana na Diwani wa Kata hiyo, George Sungura,  kwamba mazingira ya shule hiyo hayakidhi mahitaji ya msingi ya watoto waliopo hapo.

 “Tumefunga shule hii kwa kwani hapa tunazingatia usalama na ulinzi wa watoto, warudi kwa wazazi wao, halafu wataendelea kuwatafutia elimu sahihi taratibu maana hapa walikuwa wamewekwa mazingira mabovu, fedha inalipwa halafu shule haijasajiliwa,” alisema. 

Kwa upande wake mmiliki wa shule hiyo, Mchungaji Yohana  Nzuguni wa kanisa la Angalikana amekiri kosa hilo na kuomba radhi kwa serikali na ameahidi kukamilisha  ujenzi wa majengo ya shule yake ndani ya miezi miwili kwa kushirikiana na wafadhili wake ndipo aendelee na utaratibu wa kuandikisha watoto

0 comments:

Post a Comment