Help Children
Love them
Saidia Watoto

Saturday, December 15, 2012

YTN inalenga kuwapatia elimu vijana kuhusiana na ushiriki wao katika kukuza utalii

Mratibu wa kitaifa wa Young Tourism Network Richard Sempindu akifafanua jambo kuhusiana na ushiriki wa vijana katika kuendeleza na kusaidia Utalii kwa vijana.

Seriously kijana alijipanga katika kuhamasisha na kuongeza hamasa ya vijana katika kusaidia masuala ya utalii

Ni somo ambalo lilihusisha vijana
 kutoka vyuo mbalimbali nchini ambapo kwa pamoja walitoa maoni yao kuhisiana na masuala ya ushiriki wa vijana katika kukuza utalii hapa nchini
Hii ni sehemu ya washiriki hao

Amani wa Tambaza alikuwapo na wanafunzi wengine

Hapa vijana hao wakitoa maoni yao kuhusiana na nini kifanyike kusaidia kukuza utalii kwa kuwashirikisha vijana nchini


Ukafika muda wa kupata kumbukumbu zao mbele ni Esther Kway

Wanafunzi walipata picha ya pamoja

Founder and Executive Director wa Youth Tourism Network (YTN) Setty Mkisi akijadiliana jambo na Sempindu wakati wa semina hiyo.

Habari Kamili.

Hakika naweza kusema kuwa vijana wa kitanzania wanazidi kuamka katika kutaka kuleta mabadiliko katika vijana wenzao na hata jamii kwa ujumla wake.

Young Tourism Network (YTN) ni moja kati ya juhudi za vijana katika kupigania maendeleo ya vijana wenzao kuhakikisha kuwa sauti zao zinasikika lakini pia kuhakikisha kuwa wanahakikisha serikali na wanajamii kwa ujumla wanatambua umuhimu wa nguvu iliyopo kwa vijana nchini.

Setty Charles  Mkisi ni mfano wa vijana ambao wanatoa elimu mbalimbali kwa wenzao katika kuhakikisha kuwa wanafanikiwa na wanafika mbali kimaisha kwa kuwajengea uwezo.

Katika picha za hapo juu aliwashirikisha wadau mbalimbali katiak kuwapatia elimu vijana na kusikiliza maoni yao juu ya nini kifanyike katika kuhakikisha kuwa sauti zao zinasikika na kufanyiwa kazi.

Alihakikisha kuwa vijana wanatoa maoni yao juu ya nini kifanyike katika kusikilizwa na kushirikishwa kwao katika mchakato wa kimaendeleo ya sekta ya utalii hapa nchini .

Maoni ya vijana hao yatawekwa wazi katika blogu hii muda si mrefu ili kutoa nafasi ya vijana mbalimbali nanyi kushiriki.

-- Kama unalo la kuongezea katika hili tuwasiliane kwa email ya evancengingo@yahoo.com au just like page yetu ya Faceboo k na utoe maoni yako 

0 comments:

Post a Comment