UJENGAJI wa fremu
za maduka 10 mbele ya shule ni kinyume cha sheria hivyo NAIBU Waziri wa elimu
na Mafunzo ya Ufundi,Philipo Mulugo moja kati ya shule aliyoifunga ni ya Mwenyekiti
wa SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) mkoa wa Dar es salaam ,
Hassan Kaumo kwa Aidha,Waziri amehaidi kufuatilia usajili wa shule hiyo kwani
inaonekana kusajiliwa mwezi June kwa madai maduka hayo hayakuwepo wakati mwezi
Septemba Naibu waziri aliobaini kuwapi kwa maduka katika shule.
Shule hiyo
ya Awali na Msingi ya Heroes iliyoko Chanika wilaya ya Ilala imefungiwa hadi
itakapobomoa maduka hayo hao kuihamishia sehemu nyingine.
Akiwa katika
ziara ya kutembelea shule ,Mulugo alifika shuleni hapo na kufunga shule hiyo na
kumtaka mmiliki kufikia mwezi Januari asipokee wanafunzi mpaka warudishe majengo kama ilivyosajiliwa.
“ninafunga
matumizi ya shule ya elimu ya awali na msingi mpaka afike wizarani na wakaguzi
waone amefanya marekebisho au kuhamia sehemu nyingine kwani amechanganya
biashata za maduka na shule “Alisema
Mmiliki wa
shule hiyo,Kaumo alikubali kufanya makosa ya kujenga maduka na kuhaidi kufanya
marekebisho kwa kubomoa maduka wiki ijayo nakurudisha kama
ilivyokuwa mfumo wa zamani.
Anasema
Lengo lilikuwa kuwa na biashara zinazoendana na mahitaji ya wanafunzi shuleni
hapo,na alipopata taarifa ya Naibu waziri kupita na kukemea maduka shuleni
aliyafunga yote.
Katika Shule
ya Deli iliyopo Pugu ,alibaini shule hiyo kutosajiliwa lakini ikiendelea
kutangazwa kutoa elimu ya kitaifa ya shule ya awali na uangalizi maalum wa
watoto.
alipofika
shuleni hapo alikuta wakiendelea kuandika tangazo mlangoni na kuamlishwa
kulifuta kwani haijasajiliwa kutokana na eneo lake kuwa
dogo huku likizungukwa na maduka.
Aliyekuwa
Mwalimu wa taaluma shuleni hapo,Talile Hussein alikiri kutosajiliwa na kwamba awali ilikuwa
sekondari lakini baada ya kupata matatizo ya kidato cha pili mwaka jana
waliwataka wazazi kuhamisha wanafunzi wote na kubaki kituo cha twisheni.
Alisema sasa
wako katika mpango wa kuanzisha shule ya kimataifa ya awali na wamenza
kutangaza bila kusajili na katika eneo hilo
ambalo awali walikataliwa kusajiliwa kutokana na kuwa dogo.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment