KATIKA
kuhakikisha unatoa burudani kwa watu wa rika zote hadi wanafunzi hivyo ukumbi wenye hadhi
ya kimataifa wa Club Bilicanas, jumapili hii utaanza kupiga disko maalum
kwa watu wenye umri chini ya miaka 18 ‘Blue Tooth Session’ ambayo
itakuwa ikifanyika ndani ya .
Mmoja
ya viongozi wa ukumbi huo, Hamis Omari amesema kwamba , lengo ni kuwapa
burudani vijana hao ambao kutokana na umri wao hawawezi kupata fursa ya
kuhudhuria burudani zinazofanyika usiku.
Amesema
kuwa, pamoja na burudani ya muziki, vijana hao pia watapata fursa ya
kushindana katika kusaka vipaji ambapo kiingilio kitakuwa sh 3,000.
Ameonngeza
kuwa, kwa jioni mashabiki watapata burudani kutoka kwa wasanii
wanaofanya vema katika muziki wa bongo fleva kupitia usiku wa 'Bongo
Starz nite' ambapo kiingilio ni sh 6,000 kwa kila mmoja.
0 comments:
Post a Comment