huyu ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Rwanda ambae kwa sasa yupo hapa nchini kwa ziara ya kimafunzo ya muziki akishirikiana na wasanii wa hapa nchini kujifua zaidi |
Akiwa na msanii Cyril wa hapa Bongo |
Akiwa na Cyril, Ben Paul pamoja na yeye mwenyewe |
Hawa wadau wakishajipika kimuziki na wakitoa ngoma yao basi mambo yatakuwa mazuri sana |
MSANII wa muziki wa kizazi
kipya kutoka nchini Rwanda aitwae
Ngeruka Faycal amesema kuwa Tanzania ni sehemu ya kujifunzia masuala mengi yahusuyo muziki na sanaa nzima kiujumla.
Faycal alisema kuwa kwa sasa ameamua kujihusisha zaidi na wasanii kutoka Tanzania na hivyo amekuja kujifunza kwanza muziki unavyotakiwa kwenda.
Akiwa hapa nchini anatarajia kuachia wimbo wa Kiswahili na msanii mahiri wa nyimbo
za Bongo Flava Ben Paul wa hapa Tanzania.
Msanii huyo mwenye makazi
yake nchini Ubelgiji anasifika kwa uwezo wake wa kupanga sauti mbalimbali na
kwa sasa tayari ameanza mazungumzo Ben Paul kupitia meneja wake wa iliyopo
nchini Ubelgiji.
Aliliambia gazeti hili kuwa
amekuwa akifuatilia namna ambavyo Ben Paul anaimba na amekuwa akifanya vema
katika muziki huku akisisitiza kuwa kwa muda mrefu amekuwa akivutiwa na vionjo
vya muziki wa Jazz vilivyopo katika nyimbo za Ben Paul.
Naye Ben Paul wakati
akizungumza na gazeti hili alisema kuwa mpango wake kwa sasa ni kujitanua zaidi
kimuziki kwa hiyo kuimba na msani huyo wa Rwanda ni hatua moja wapo ya
kutimiza ndoto zake.
“ Mimi naona kuwa kwa sasa
huyu msanii ni msanii ambae anaweza kuimba kila aina ya sanaa na pia naona kuwa
kwa sasa kuna uwezekano wa kufanya kazi pamoja ila ndio mazungumzo yanaendelea
kati ya meneja wangu na wa Code” alisema Ben Paul.
--- -------
0 comments:
Post a Comment