Add caption |
Wanamitindo waliwakilisha pia katika kuchangisha fedha hizo |
Habari Kamili
Na Evance Ng’ingo
ONESHO la mavazi kwa lengo la
kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia watoto waishio katika mazingira
hatarishi juzi lilikusanya shilingi milioni 72
kwa njia ya mauzo ya nguo na vitu vya thamani.
Onesho hili liitwalo Red
Ribon liliandaliwa na mbunifu wa mavazi Khadija Mwanamboka kwa kushirikiana na
Flaviana Matata Foundation ambapo ilihudhuriwa na watu wengi.
Vitu vilivyouzwa ni pamoja na
vinyago, nguo za kisasa, nguoz zilizobuniwa na wabunifu wa ndani, vitabu na
bidhaa nyinginezo muhimu.
Akizungumzia mafanikio
yaliyopatikana kutokana na michango itokanayo na onesho hilo
la mavazi kwa miaka mitano Kadija alisema kuwa wanawahudumia watoto katika
vituo vya Magomeni na Kigamboni ambapo wanatoa misaada kwa watoto mbalimbali.
Alisema kuwa kupitia mauzo ya
kazi mbalimbali za wabunifu wa mavazi wameweza kupata fedha kwa njia ya mauzo
ya nguo na watu wengi wametoa misaada yao.
Katika mauzo ya jana Mbunge
wa Kigoma Kaskazini Zito Kabwe alichangia kwa kununua kitabu kwa shilingi
milioni 3 ambapo pia alichangamsha hafla hiyo baada ya kuimba wimbo wa leta
tutigite akiwa na msanii Linex.
Watu wengine mbalimbali
walichangia fedha jana kwa njia mbalimbali ambapo Mkurugenzi wa Benchmark
Production Ritha Paulsen alinunua gauni lililotolewa na mbunifu wa mavazi
Evelyn Rugemalila wa Eve Collection kwa shilingi milioni 2
Mwisho
0 comments:
Post a Comment