Mfugale akimkabidhi mwakilikishi wa TBC 1 zawadi kwa kuonesha inshara ya shukrani kutokana na msaada wa Redio hiyo katika kukuza biashara zake |
Mmiliki wa hoteli hiyo Mfugale akitoa neno la shukrani kwa waandishi kuwashukuru kwa msaada wao katika kusaidia kukuza biashara zake za hoteli |
Mwandishi wa Chanel Ten Kibwana Dachi akitoa neno la shukrani kwa niaba ya waandishi waliohudhuria |
Waandishi walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali siku hiyo kabla ya kuanza ziara ya kutembelea vyumba vya hoteli yake mpya |
Hiki ni chumba chenye hadhi ya kidiplomasia |
Mfugale aliongozana na waandishi hadi vyumbani ambapo alipata fursa ya kuwafafanulia masuala mbalimbali |
Sehemu za ndani za vyumba hivyo |
Mahala pa kunawa mikono |
Hapa akiwaonesha jakuzi lililopo katika moja ya vyumba vya hoteli hiyo |
Ulifika wakati wa kusakata muziki ambapo wafanyakazi na waandishi kwa pamoja walicheza |
Wafanyakazi wa East Africa Television wakiwa na Mfugale |
Habari Kamili
MMILIKI wa hoteli za Peacock
nchini Joseph Mfugale ametoa elimu kwa wajasiriamali wanaochipukia kuepuka kukata tamaa na badala yake wajikite zaidi katika kujiendeleza kielimu na kibiashara kiujumla.
Alisema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya miaka 20 tangia kuanzishwa kwa hoteli yake ya Peacock iliyopo Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Akizungumzia mikakati ya maendeleo ya hoteli zake Mfugale alisema kuwa kwa sasa anampango wa kujenga hoteli ya
nyota tano katika eneo la Kigamboni itakayokuwa na uwanja wa gofu humohumo.
Mfugale alisema hayo juzi
wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika hafla fupi ya
kusherehekea miaka 20 tangia kuanzishwa kwa hoteli ya Peacock iliyopo Mnazi
Mmoja, Dar es salaam.
Mfugale alisema kuwa kwa sasa
biashara ya hoteli inazidi kukua kwa kasi hapa nchini na kuna kila sababu kwa
wawekezaji wazawa kuhakikisha kuwa wanawekeza katika sekta hiyo iliyoajili watu
wengi.
Alisema kuwa kwa kipindi cha
miaka 20 tangia kuanzishwa kwa hoteli ya Peacock ya Mnazi Mmoja tayari amepanua biashara za
hoteli kwa kujenga jengo jipya la hoteli hiyo lililopo nyuma ya hoteli hiyo lenye vyumba.
Alisema kuwa pia anaendelea
na ujenzi wa jengo la Peacock lililopo Iringa mjini ambalo lotaisaidia kuongeza
ajira kwa vijana katika mkoa huo pamoja na kuwahifashi watalii.
Waandishi wa habari walipata
fursa ya kutembelea vyumba vya jengo jipya la Peacock la Mnazi Mmoja ambapo
kuna vyumba vya hadhi ya raisi, wanadiplomasia pamoja na watu wa kawaida.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment