Huyu ni mmoja kati ya wanawake waliopanda Mlima Kilimanjaro yeye ni Mtanzania |
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Utalii ya nchini Nepal
Subash Niroula akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Utalii wa Wizara ya
Maliasili na Utalii Ibrahim Mussa wakati wa hafla ya kuwaaga wanawake saba
kutoka nchini Nepal waliopanda Mlima Kilimanjaro katioka maadhimisho ya siku ya
wanawake duniani
Mkurugenzi wa Utalii wa Wizara ya Maliasili na Utalii Ibrahim Mussa akizungumza katika hafla hiyo |
Picha ya pamoja na wanawake waliopanda mlima huo |
Musa na mkewe huyo wa katikati |
Mimi pia nilipiga picha na wanawake hao |
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Aloyce Nzuki na Mkurugenzi wa Utalii wa Wizara ya Maliasili na Utalii Ibrahim Mussa wakiwa katika picha ya pamoja katikati ni Mrs Mussa
KIONGOZI wa kundi la Wanawake Saba kutoka nchini Nepal waliopanda mlima Kilimanjaro, Shailee Basnet,
ameitaka serikali pamoja na wanajamii kusaidia kupambana na manyanyaso dhidi ya wanawake nchini.
Alisema kuwa
katika kusaidia kampeni dhidi ya manyanyaso ya wanawake duniani wamekuwa na
utamaduni wa kupanda milima mirefu duniani na kufikisha ujumbe wa kutetea haki
za wanawake ambapo wameshapanda milima Everest na Mlima Kilimanjaro.
Alisema kuwa wakiwa hapa nchini wametembelea shule mbalimbali kutoa elimu ya kujiamini na kujitambua kwa wanafunzi wa shule mbalimbali.
Wakati huohuo Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Bodi ya Utalii ya nchini Nepal Subash Niroula alisema kuwa tayari
wamenza kukutana na wamiliki wa kampuni za Utalii za hapa nchini.
Niroula
alisema kuwa Tanzania kuna vivutio vingi vya utalii ambavyo vinatakiwa
kutangazwa nchini Nepal na sehemu nyingine duniani.
Alisema kuwa
ili kufanikisha utangazwaji wa utalii huo kunahitajika kuwepo kwa juhudi
binafsi kutoka kwa wadau wa utalii wa Nepal na Tanzania kushirikiana pamoja ili
kufanikisha ukuaji wa utalii huo.
Alisema kuwa
Mlima Kilimanjaro unafahamika zaidi nchini Nepal na unaweza kutangazwa
kikamilifu zaidi ili kuongeza idadi ya watalii wanafika Tanzania.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment