Akimuonesha kitabu hicho Professor Esther Mwaikambo |
Faraja Kotta Nyarandu akitoa maoni yake kuhusiana na kitabu hicho
Wanafunzi wakifuatilia kwa umakini wa hali ya juu
Hao ndio wahusika wakuu wa kitabu hicho
Nancy na Faraja
Nancy akisaini kitabu chake
Wakaanza kukisoma wanafunzi
Ilikuw furaha kwa wanafunzi
MLIMBWENDE
wa Tanzania mwaka 2005 Nancy Sumari jana alizindua kitabu kiitwacho Nyota Yako
alichokitunga mwenyewe chenye ujumbe wa kuwahamasisha wasichana masuala
mbalimbali yanayowahusu ikiwa pamoja na kutoa ujumbe mbalimbali wenye kulenga
kusaidia kuwaepusha na hatari mbalimbali.
Akizungumza
wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho Nancy alisema kuwa akiwa kama
mlimbwende pia mwanaharakati wa haki za wasichana ameona kuwa kuna kila sababu
ya kuzungumza na wasichana wa Tanzania nzima kwa njia hiyo.
Alisema kuwa
kitabu hicho chenye kurasa 26 kinaelezea nafasi ya mwanamke katika jamii ya
kitanzania, uwezo wa mtoto wa kike, Umuhimu wa namna ya kujithamini, kuweka
malengo, ndoto na maazimio, kujiamini kujiendeleza kimalengo.
Katika uzinduzi
huo uliohudhuriwa na wadau wengi wa elimu nchini pia uluhudhuirwa na mshindi wa
Tuzo ya JMartin Luther King Esther Mwaikambo
ambae pia mbali na kumpongeza Nancy aliwasihi wasichana wenye mafanikio nchini
kuwa na shauku ya kuwasaidia wasichana wengine wenye kutaka kutumiza ndoto zao.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment