WAZIRI Mkuu
mstaafu, Edward Lowassa amepongeza wazazi wa wanafunzi wa shule ya wasichana ya
masista wa Kikatoliki Henry Gogarty
iliyopo wilayani Arumeru kwa jitihada za kujenga majengo ya shule hiyo kwa
hiari.
Alisema
mfano huo unapaswa kuigwa na wazazi wa shule nyingine.
Lowassa
alisema hayo juzi kabla ya harambee ya ujenzi wa maabara na mabweni ya shule
hiyo. Alisema kuwa wazazi wengine wanapaswa kuiga mfano huo.
Alisema
pongezi anazotoa ni za dhati,
zinazopaswa kuigwa na wazazi wengine kwani katika harambee nyingi alizowahi
kufanya, hajawahi kuona wazazi wanaoweza kujitoa kwa kiasi kikubwa kuchangia
harambee na maendeleo ya shule.
"Hawa
wazazi wanapaswa kupongezwa na mfano huu unapaswa kuigwa katika shule zingine,
kwani wengi wamekuwa wakitaka kuchangiwa tu, tofauti na hapa wazazi wanachanga
wenyewe hivyo wanapaswa kupewa nguvu kubwa,’’alisema.
Pia,
Lowassa alilisifu shirika la masista wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa jitihada zake
za kuendeleza elimu hapa nchini na nje ya nchi.
Alisema na kuisifu shule hiyo katika kufanya vizuri
katika mitihani yake ya Taifa. Aliwataka walimu kuendelea na moyo huo ili shule
hiyo iweze kuongoza kitaifa.
Mkuu
wa Shule hiyo, Bernada Moshi alisema shule hiyo ilianzishwa mwaka 2011 na inakabiliwa
na changamoto kubwa za uhaba wa mabweni kwa ajili ya wanafunzi wa kike na
maabara.
Moshi
alisema lengo ni kukusanya Sh milioni 250 kwa kujenga majengo ya mabweni na
maabara. Alisema lengo kuu la shule hiyo ni kutoa elimu bora na maadili kwa mtoto
wa kike, ambaye ni nguzo muhimu katika maendeleo ya familia na jamii.
Katika harambee
hiyo, jumla ya Sh196,493,350 zilichangwa, huku fedha taslimu zikiwa Sh
120,863,350 na ahadi Sh 75,630,000.
Lowassa
pamoja na rafiki zake walitoa Sh milioni 10 na kompyuta mbili.
0 comments:
Post a Comment