Mwanaharakati
wa haki za wanawake na watoto Tery Gbemudu, Mama Terry, akiagana na Rais Mstafaau wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi juzi wakati
wa uzinduzi wa kipindi cha luninga cha kiitwacho Pamoja Tunaweza cha Mama Terry.
Mdau wa elimubora
MWANAHARAKATI
wa muda mrefu katika masuala ya haki za wanawake pamoja na mapambano dhidi ya
maambukizi ya virusi vya Ukimwi, Tery Gbemudu, Mama Terry, amezindua kipindi
chake cha Luninga kiitwacho Pamoja Tunaweza chenye kuendeleza mapambano dhidi
ya uhalifu.
Kipindi
hicho kilizinduliwa juzi na rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi katika bwalo la
Police Officers Mess lililopo Oysterbay, Dar es salaam na kudhuriwa na wakuu
mbalimbali wa jeshi la Polis aliwamo Inspekata Jenerali Said Mwema.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya uzinduzi huo Mama Tery alisema kuwa kipindi
hicho kitakuwa kikirushwa katika stesheni ya TBC mara mbili kwa wiki.
Alisema kuwa
kipindi hicho kinalenga kuwafundisha wanajamii namna ya kuepuka na kupambana na
uhalifu ambao unaonekana kuwa unazidi kuota mizizi hapa nchini.
Alisema kuwa
ili kuweza kuieleimisha jamii ya sasa masuala mbalimbali ya kupambana na
uhalifu ni lazima uwafuate katika misingi ya kisasa ambapo anaona kuwa kwa
kutumia kipindi cha Luninga ni njia mojawapo ya kuwafikia kirahisi.
Alisema kuwa
kipindi hicho cha dakika 90 kinagusa nyanja zote za ulinzi na usalama ambapo
wanahojiwa watu wa mitaani kuhusiana na wanavyoathiriwa na uhalifu lakini pia
kunakuwa na watu ambao watakuwa studio wakihojiwa na kufafanua hoja mbalimbali
kuhusiana na uhalifu.
“ Kwa hiki
ni kipindi cha kurekodi ambapo watu mbalimbali wanahojiwa na kueleza ulewa wao
wa masuala ya uhalifu lakini pia kunakuwa na wau ambao wanafafanua uhalifu huo
kiundani na kuangalia namna ya kuwasaidia wote kiujumla” alisema Mama Terry.
Akisoma
hotuba ya Rais Mstaafu Mwinyi ambae alifika kweye eneo hilo lakini alipata
udhuru, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meki Sadik alisema kuwa kipindi
hicho kitakuwa ni chachu yamabadiliko.
Alisema kuwa
katika jamii ya sasa iliyobadilika na kuathiriwa na utandawazi inatakiwa kuwepo
na watu ambao wanabuni njia za kisasa za kuelimisha mapambano dhidi ya uhalifu.
Kipindi
hicho pia kinaendeshwa kwa msaada wa jeshi la Polis ambapo IGP Mwema amempatia
ofisi katika bwalo hilo la Police Officers Mess ambayo Mama Tery anaitumia
kufanyia kazi zake kurekodia pia.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment