|
Hapa akijadiliana jambo na wadhamini wake kabla hawajampatia msaada huo |
|
Akiingia ukumbini |
|
Akila chakula na watoto wake |
|
Akiwa na wakurugenzi wa Taasisi yake |
|
Kwa sababu yeye ni msanii basi aliimba na watoto wake hao wimbo ulitia huruma sana |
|
Akipokea msaada huo kutoka kwa kampuni ya Sayed Corporation LTD |
|
Hapa ni wakati akiagana na mgeni rasmi ambae alikuwa Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Husein Mwinyi |
|
Hapo akipokea baiskeli zenyewe |
|
Akatoa hotuba yake makini |
|
Mmoja kati ya wakurugenzi wa taasisi hiyo akizungumza |
|
Akiagana na ofisa kutoka ubalozi wa Pakistan |
|
Group picha |
|
Group picture na watoto wa kituoni |
|
|
|
|
|
|
|
WAZIRI wa
Afya na Ustawi wa Jamii Dk Hussein Mwinyi juzi alikabidhi hundi ya shilingi
milioni 10 pamoja na baiskeli 30 kwa Taasisi ya Vicky Foundation inayomilikiwa
na Mbunge wa Viti Maalum Vicky Kamata.
Akikabidhi
msaada huo uliotolewa na kampuni ya Sayed Corporation LTD Mwinyi alisema kuwa
serikali inatambua na kuheshimu juhudi zinazofanywa na makampuni pamoja na
mashirika mbalimbali katika kusaidia jamii.
Alisema kuwa suala la watoto wa mitaaani, yatima
pamoja na kuwasaidia wajane ni suala muhimu ambalo linahitaji ushirikiano wa
dhati kutoka kwa wanajamii na mashirika kama anavyofanya Mbunge Vicky Kamata.
Naye Mbunge
huyo alisema kuwa msaada huo ni muhimu kwake kwa kuwa unawasaidia watoto kadhaa
wanaolelewa na Taasisi hiyo.
Alisema kuwa
ana watoto walemavu, watoto yatima pamoja na wenye mahitaji maalum ambapo
alisema kuwa msaada huo unaweza kusaidia katika kupunguza changamoto kadhaa
zinawazowakabili.
“ Hii
Taasisi yetu makao makuu yake yapo mkoani Geita na tumekuwa tukikabiliwa na
changamoto mbalimbali ambapo kwa sasa tunaona kuwa kuna mwanga mkubwa mbele
yetu ambao tunatakiwa kuupata na ili kuupata mwanga huo ni vema tukashirikiana
watu wote kwa pamoja” alisema Vicky.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment